Nenda kwa yaliyomo

Amina Khoulani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

'

Amina Khoulani
Alichaguliwa kuwa Mwanamke wa Kimataifa Jasiri mnamo Machi 2020. Tuzo zilizotolewa tarehe 4 Machi 2020 - Amina Khoulani
Kazi yakeMwanaharakati


Amina Khoulani (kwa Kiarabu: أمينة خولاني) ni mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka nchi ya Syria na muathirika wa jela za Assad, anayejulikana kwa kazi yake ya kutetea wafungwa wa kisiasa na familia zao. Alihamia uhamishoni huko Manchester, Uingereza, mnamo mwaka wa 2014. Tangu wakati huo, amekuwa akifanya kampeni kwa ajili ya wafungwa wengine na kusaidia familia zao. Alikuwa mshindi wa Tuzo ya Kimataifa ya Wanawake wa Ujasiri mwezi Machi 2020.[1]

Maisha yake

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2013 alikamatwa baada ya kufanyika maandamano ya amani nchini Syria. Angefunga miezi sita lakini mume wake angefungwa kwa miaka miwili na nusu gerezani kwenye gereza la Sednaya. Wasyria 140,000 walipelekwa gerezani bila kushtakiwa na ndugu zake watatu walifariki gerezani.[2]

Mwaka wa 2014 aliondoka Syria. Khoulani alijitolea kampeni ya kuachiliwa huru kwa wafungwa wengine wa Syria na mwaka wa 2017 alikuwa mmoja wa waanzilishi wa "Families for Freedom". Shirika hilo lenye makao yake Uingereza linasaidia familia za wale waliozuiliwa au waliopotea.[3]

Aliteuliwa kama Mwanamke Shujaa wa Kimataifa mnamo Machi 4, 2020, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani. Baada ya sherehe, alihudhuria katika Birmingham, Alabama.

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Ameolewa, pia ana watoto watatu na wanaishi Heald huko Manchester. [4]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Amina Khoulani kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.