Alphonse Menyo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Alphonse Menyo ni mwigizaji wa Ghana.[1]anafahamika zaidi kwa uhusika wake katika filamu za Freetown na Gold Coast Lounge.[2]

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa Accra, Ghana. Baba yake, Bernard Menyo, alitokea Afrika Mashariki na aliwahi kuwa mwanafunzi wa National Film and Television Institute (NAFTI). Bernard alishinda tuzo kwenye Panafrican Film and Television Festival of Ouagadougou (FESPACO) kutokana na filamu ya Whose fault. Mama yake Menyo, Eugenia, ametokea Ghana ana fanya kazi katika shirika lisilo la kiserikali.[2]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Menyo alihudhuria akademi ya uigizaji filamu ya Ghallywood Accra kusomea sinema na maigizo. Alianza kazi yake ya uigizaji mwaka 2009 kwa kuigiza jukwaani. Mwaka 2015 alikuwa muhusika katika filamu ya Freetown kuhusu uhuru wa Marekani, iliyoongozwa na Garret Batty.[3] Filamu hiyo ilionyeshwa mara kadhaa katika matamasha ya kimataifa ya filamu na iliteuliwa mara kadhaa katika tuzo za filamu za Ghana.[4]

Menyo aliigiza filamu yake ya kwanza ikijulikana kama Utopia. Filamu hiyo ilipata teuzi nne katika tuzo za filamu za Ghana. Mwaka 2017, Utopia ilikua filamu pekee ya Ghana iliyochaguliwa kuonyeshwa katika maonyesho ya filamu ya Helsinki HAFF.

Filamu[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Filamu Uhusika Aina Marejeo.
2015 Freetown Meyers Filamu
2017 Black Rose Daniel Filamu fupi
2020 Gold Coast Lounge Daniel Filamu

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Biofilm.png Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alphonse Menyo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.