Alphonce Kyessi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Alphonce G. Kyessi (alizaliwa Mkoani Kilimanjaro), ni profesa, mtafiti na mshauri katika fani ya upangaji miji, maendeleo na usimamizi wa makazi ya watu. Kwa sasa ameajiriwa kama Profesa Mshiriki wa muda katika Taasisi ya Mafunzo ya Makazi ya Watu katika Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), Dar es Salaam ambako amekuwa akifanya kazi tangu mwaka 1993.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 1980 alipata Diploma ya Juu ya Mipango Miji na Vijijini katika Chuo Kikuu cha Ardhi na Mafunzo ya Usanifu (Taasisi ya Ardhi), leo Chuo Kikuu cha Ardhi. Mwaka 1985, alipata Diploma yake ya Uzamili ya Tafiti za Miji ikiwa ni pamoja na Mifumo ya Taarifa za Kijiografia katika Taasisi ya Utafiti wa Anga na Sayansi ya Ardhi (ITC), Enschede, nchini Uholanzi. Pia alipata Shahada yake ya Uzamili ya Sayansi ya Tafiti za Miji na Uchambuzi wa Makazi ya Watu ikiwemo Jiografia na Mifumo ya Habari katika Taasisi ya Utafiti wa Anga na Sayansi ya Ardhi (ITC). Mnamo 2001, alimaliza PhD yake ya Upangaji wa Maeneo na Miundombinu katika Chuo Kikuu cha Ufundi cha Dortmund, Ujerumani.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Ardhi, alifanya kazi na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa miaka 13 kati ya 1980 na 1992. Amekuwa akifanya uchambuzi wa makazi ya watu, umaskini wa mijini, usafiri wa umma mijini, kilimo cha mijini, mipango na usimamizi wa mazingira ya miji na mifumo ya habari za kijiografia (GIS) katika upangaji na usimamizi wa miji. Machapisho yake ya utafiti na ushauri yanazingatia mabadiliko ya hali ya hewa, sera ya umma, makazi, udhibiti wa ardhi hasa wa makazi yasiyo rasmi, huduma ya ardhi, upangaji wa miundombinu na maendeleo hasa usimamizi wa kijamii na ushiriki wa jamii na kilimo cha mijini. [1]

Nafasi za heshima[hariri | hariri chanzo]

Kyessi ni Katibu wa Heshima wa Chama cha Washauri Tanzania na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Mashujaa iliyopo kata ya Sinza jijini Dar es Salaam.[2] [3] [4] [5] [6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Educators advice on teaching students to compete in labour market" (kwa Kiingereza). The Citizen. 6 July 2014. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-06-27. Iliwekwa mnamo 28 June 2023.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. "Alphonce G. Kyessi - INTERACT-Bio". interactbio.iclei.org. 
  3. "Benki ya CRDB yakabidhi madarasa na madawati katika manispaa ya ubungo" (kwa Kiswahili). Ubungo Municipal Council. 22 September 2022. Iliwekwa mnamo 28 June 2023.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  4. "BENKI YATOA MSAADA WA MADARASA NA MADAWATI SHULE SEKONDARI MASHUJAA" (kwa Kiswahili). Mtaa Kwa Mtaa. 3 February 2022. Iliwekwa mnamo 28 June 2023.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  5. Michuzi, Issa (3 February 2022). "Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Mashujaa, Prof. Alphonce Kyessi". Iliwekwa mnamo 29 June 2023.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  6. Dande, Francis (22 Oktoba 2022). "SHULE YA SEKONDARI MASHUJAA YAFANYA MAHAFALI YA KWANZA 2022". Iliwekwa mnamo 29 June 2023.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alphonce Kyessi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.