Nenda kwa yaliyomo

Almere

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru






Almere

Bendera
Almere is located in Uholanzi
Almere
Almere

Mahali pa mji wa Almere katika Uholanzi

Majiranukta: 52°22′18″N 5°13′15″E / 52.37167°N 5.22083°E / 52.37167; 5.22083
Nchi Uholanzi
Mkoa Flevoland
Idadi ya wakazi (2010)
 - Wakazi kwa ujumla 188,209
Tovuti:  almere.nl
Mji wa Almere

Almere ni mji na manispaa ya mkoa wa Flevoland, nchini Uholanzi. Mji umepakana na Lelystad na Zeewolde. Ndani ya manispaa ya Almere kuna wilaya ya Almere Stad, Almere Haven, Almere Buiten, Almere Hout, Almere Poort (bado inajengwa) na Almere Pampus (ipo katika hatua ya usanifu).

Almere ni mji mdogo nchini Uholanzi: nyumba ya kwanza ilimalizika mnamo 1976, na Almere ikawa manispaa mnamo 1984. Ni manispaa kubwa sana katika Flevoland ikiwa na idadi ya wakazi takriban 184,405 (7 Julai 2008)[1], na mji wa 8 kwa ukubwa nchini Uholanzi[2]. Mnamo mwezi wa Oktoba 2007, halmashauri ya jiji ya Almere imekubaliana na serikali kupanua mji na kufikia kuwa na wakazi wapatao 350,000 hadi ifikapo mwaka wa 2030.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mipango ya awali ya IJsselmeerpolders aliona ardhi ikitumika kwa ajili ya kilimo. Hata hivyo, baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia ujenzi wa majumba ulihitajika kwa ukuzaji haraka wa idadi ya watu mjini Amsterdam na miji miwili ilipangwa katika sehemu za ardhi ya Oostelijk Flevoland na Zuidelijk Flevoland. Mji katika eneo la Oostelijk Flevoland likawa Lelystad. Mji katika eneo la Zuidelijk Flevoland uliendelea kuita Zuidweststad (Kiswahili: Mji wa Kusini Magharibi) katika hatua za mwanzoni, lakini katika miaka ya 1970 mji ukawa Almere, umepewa jina baada ya jina la zama za kati la Zuiderzee. Nyumba ya kwanza mjini Almere ilimalizwa mnamo 1976. Kwa kipind hicho mji bado ulikuwa ukimilikiwa na Openbaar Lichaam Zuidelijke IJsselmeerpolders (Z.IJ.P.), ikiwa na Landdrost. Mnamo mwaka wa 1984 Almere ikapata kuwa manispaa rasmi. Awali, Almere ulitazamiwa kama mji wenye vituo kedekede. Wazo hili lilitelekezwa hapo baadaye kwa hisani ya kuwaruhusu majirani kama vile Tussen de Vaarten kujenga makazi yao mjini hapa. Pia kuna tofauti kadhaa katika mtindo wa ujenzi wa majumba ya sasa na yale ya zamani katika baadhi ya maeneo ya mji huu. Mpango wa ujenzi wa majumba ya mjini Almere kunako miaka ya 1970s ulikuwa wa pamoja na uliangalia sana hadhi ya usawa kijamii. Hata hivyo, kuanzia miaka ya 1990 majumba ya hali ya juu yalijengwa huku yakipishana na mfumo wa ujenzi (mfano kwenye Regenboogbuurt).

Demografia

[hariri | hariri chanzo]
Theater "Schouwburg Almere"
  Almere Haven Almere Stad Almere Buiten Almere Hout Almere Poort Almere Pampus Almere in total
1970             52
1975             47
1980 6596           6632
1985 21410 17240 1559       40297
1990 22355 37024 11499       71087
1995 22376 58816 22740 564     104496
2000 22237 83934 35290 1336     142797
2005 22590 103560 47358 1366     175008
2007 22507 105261 51751 1345 134   180998
  1. (Kiholanzi) CBS Statline. Retrieved on 2008-06-09.
  2. (Kiholanzi) CBS Statline - Bevolking; ontwikkeling in gemeenten met 100 000 of meer inwoners. Retrieved on 2008-06-09.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: