Nenda kwa yaliyomo

Albuquerque, New Mexico

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mji wa Albuquerque, New Mexico


Albuquerque

Bendera
Albuquerque is located in Marekani
Albuquerque
Albuquerque

Mahali pa mji wa Albuquerque katika Marekani

Majiranukta: 35°06′39″N 106°36′36″W / 35.11083°N 106.61000°W / 35.11083; -106.61000
Nchi Marekani
Jimbo New Mexico
Wilaya Bernalillo County
Idadi ya wakazi (2008)
 - Wakazi kwa ujumla 521,999
Tovuti:  www.cabq.gov

Albuquerque ni mji mkubwa wa jimbo la New Mexico nchini Marekani. Kuna wakazi 484,246 (2004) na pamoja na rundiko la mji ni 712,000. Mji upo m 1,619 kutoka juu ya usawa wa bahari.

Mji uko katika eneo kati ya mto Rio Grande na milima ya Sandia.

Eneo la Albuquerque liliwahi kukaliwa na Maindio tangu mwaka 1100. Mnamo mwaka 1540 conquistador Mhispania wa kwanza Francisco Vásquez de Coronado alipita hapa mara ya kwanza akitafuta mji ya dhahabu.

Mji uliundwa na walowezi Wahispania 1706 na kupewa jina kwa heshima ya Francisco Fernández de la Cueva mtemi wa Albuquerque na mfalme mdogo wa Hispania Mpya. Pamoja na eneo lote la New Mexiko mji ulihamishwa chini ya Marekani katika karne ya 19.

Kitovu cha kihistoria bado kina majengo ya zamani ya Kihispania. Kuna pia wakazi wengi kidogo wenye asili ya Kihispania na wengine huendelea kutumua lugha ya Kihispania.

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Albuquerque, New Mexico kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.