Alama ya uakifishaji
Alama za uakifishaji ni alama zinazotumiwa wakati wa kuandika pamoja na herufi. Kazi yao ni msaada wa kuelewa matini vema, na kudokeza maana maalumu ya maneno au sehemu za sentensi na kuonyesha muundo wa sentensi.
- . inaitwa nukta
- , inaitwa Koma au mkato
- ? inaitwa alama ya kuuliza
- ! inaitwa alama ya mshangao
- ' inaitwa apostrofi au ritifaa
- " inaitwa alama za dondoo
- : inaitwa nuktambili
- ; inaitwa nuktamkato
- - inaitwa alama ya kistari
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- Alama za Uakifishaji, Paneli ya Kiswahili, tovuti ya swa.gafkosoft.com