Nenda kwa yaliyomo

Al-Qairawin

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa ndani wa msikiti ya Al-Qairawin

Chuo Kikuu cha Al-Qairawin (kiarabu: جا معة القرويين) mjini Fes (Moroko) kiliundwa mwaka 859 kama madarasa kwenye msikiti ya Al-Qairawin. Inasemekana ni chuo kikuu cha kale kabisa duniani inayoendelea kufanya kazi hadi leo. Kuundwa kwake kulitokea miaka 70 kabla ya Chuo Kikuu cha Al-Azhar mjini Kairo (Misri).

Kati ya wanafunzi wake mashuhuri alikuwa mwanafalsafa Myahudi Maimonides.