Nenda kwa yaliyomo

Ajali ya Helikopta ya Polisi 2012, Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Helikopta iliyoanguka

Ajali ya Helikopta ya Polisi 2012 nchini Kenya ilihusisha ndege iliyoanguka ya aina ya helikopta iliyomilikiwa na polisi ya Kenya mnamo 10 Juni, 2012. AS350 Eurocopter ilianguka katika eneo la Ng'ong, na kuua abiria wote sita na wafanyakazi waliokuwepo. Kati ya walioaga dunia ni aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani na Usalama wa Kenya George Saitoti na Waziri wake Msaidizi Joshua Orwa Ojode.

Ajali[hariri | hariri chanzo]

AS350 Eurocopter iliondoka kutoka Uwanja wa Ndege wa Wilson, jijini Nairobi kwa safari kuelekea Ndhiwa ikiwa na usaidizi kamili wa Maafisa wawili wa Polisi wa Kenya kama marubani na abiria wanne: maafisa wawili wa serikali na maafisa wa Polisi waliofanya kazi kama walinzi wao. Mawasiliano ya mwisho ya redio na helikopta yalikuwa dakika tano baada ya kuondoka uwanja wa ndege wa Wilson saa 8:32 asubuhi masaa ya Kenya, halafu ndege hiyo ikatoweka kutoka kwa rada na baada ya dakika nyingine tano baadaye saa 8:42 asubuhi.Ilikuwa imeanguka katika eneo la Kibiku kwenye msitu wa Ngong nje tu ya Nairobi na kushika moto. Abiria wote sita waliuawa katika ajali;ndege ilikuwa imeharibika kabisa baada ya ajali, moto ulizuka baada ya kuanguka na kuchoma wahasiriwa "zaidi ya utambuzi". Waziri wa Usafiri, Amos Kimunya alitoa taarifa kuwa hali ya hewa ilikuwa "ya kawaida" wakati wa kuanguka kwa ndge hiyo na kulikuwa na muonekano wa kilomita 8 (5.0 mi).

Ndege[hariri | hariri chanzo]

Helikopta iliyoanguka, Eurocopter AS350 mkia nambari 5Y-CDT iliyotengenezwa viwandani mwaka 2011, ilikuwa imeenda safari kwa takriban masaa chini ya 100 wakati iliingia kuhudumia Polisi wa Kenya mwezi Januari mwaka 2012 na alikuwa kusanyiko la zaidi ya masaa 240 ya kusafiri angani tangu wakati huo.Ilikuwa imenunuliwa ili kuchukua nafasi ya helikopta nzee Mil Mi-17 za tawi la Polisi wa Kenya wa Angani.

Mpango wa safari[hariri | hariri chanzo]

Helikopta ilikuwa katika safari kutoka Nairobi hadi kijiji cha Ratang'a katika eneo la mbunge la Ndhiwa, Wilaya ya Homa Bay. Mawaziri wawili walikuwa wameabiri - Waziri wa mambo ya Ndani na Usalama George Saitoti, ambaye alikuwa ametangaza nia yake ya kugombea urais nchini Kenya, na Naibu wake Joshua Orwa Ojode - walikuwa wamepanga kuhudhuria mchango wa fedha katika Kanisa Katoliki la Nyarongi. Wawili hao walikuwa wahudhuria Misa, ambayo ilikatishwa na mkuu wa Wilaya na mkuu wa polisi Homa Bay, baada kutoa Habari kuhusu vifo vya wale wanaosubiri kuwasili kwao, ikiwa ni pamoja na mama na ndugu wengine wa karibu wa Joshua Orwa Odoje.