Aili Venonya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Aili Venonya (1963–2022) alikuwa mwanasiasa wa Namibia ambaye alihudumu kama mjumbe wa mamlaka ya kikanda wa Jimbo la Moses Garoëb.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Venonya alianza kufanya kazi kama mpishi katika Hoteli ya Kalahari huko Windhoek, Namibia. Safari yake ya kisiasa ilianza alipochaguliwa kama kiongozi wa sehemu ya SWAPO katika jimbo la Moses Garoeb mnamo mwaka 2003. Akiwa mwanachama wa chama cha SWAPO, alihudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya Swapo, ikiwa ni pamoja na mhazini wa wilaya, afisa wa habari na ushawishi na msimamizi. Alihudumu kama mjumbe wa mamlaka ya kikanda wa Jimbo la Moses Garoëb tangu mwaka 2020 hadi kifo chake mnamo mwaka 2022 [1].

Venonya alikuwa mwanzilishi na mkurugenzi mkuu wa Huduma za Chakula na Mafunzo ya Aili, ambayo ilianzishwa mwaka 2010.>


Kazi za Jamii[hariri | hariri chanzo]

Venonya alikuwa mchango wa kujitolea wa Reach for Recovery katika Cancer Association of Namibia, mpango wa kupona unaoungwa mkono na wagonjwa wa saratani ya matiti ambao wanatoa mkono wa msaada na mtandao katika mapambano dhidi ya saratani ya matiti.[2] Venonya alihudumu kama mwanachama wa bodi katika Kituo cha Jamii cha Ombili.


Kutambuliwa[hariri | hariri chanzo]

Alipongezwa na Rais Hage Geingob kwa michango yake katika sekta ya ukarimu na maendeleo ya kijamii ya Jimbo la Moses Garoeb.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://nbcnews.na/taxonomy/term/7310
  2. https://neweralive.na/posts/tributes-pour-in-for-late-councillor-venonya
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Aili Venonya kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.