Agatha Tiegel Hanson
Agatha Tiegel Hanson (14 Septemba 1873 – 17 Oktoba 1959) alikuwa mwanamke wa pili kuhitimu kutoka Chuo cha Kitaifa cha Viziwi (jina rasmi la Gallaudet College hadi mwaka wa 1894) mnamo mwaka wa 1893 na mwanamke wa kwanza kupokea Shahada ya Kwanza ya Sanaa kutoka chuoni hapo. Alifanya kazi kama mwelekezi wa wanafunzi wa viziwi na alitetea jamii ya viziwi katika maisha yake yote. Hanson pia aliandika mashairi na kuhariri gazeti kwa ajili ya viziwi.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Agatha Tiegel alizaliwa 14 Septemba 1873 huko Pittsburgh, Pennsylvania .[1] Akiwa na umri wa miaka saba alikumbwa na ugonjwa wa meningitis ya uti wa mgongo, ambao ulimsababishia kuwa kipofu na kiziwi .
Alianza kwa kusoma shule binafsi ya Kikatoliki akiwa na umri wa miaka tisa, na alipokuwa na umri wa miaka kumi na tatu alihama na kwenda kusomea Shule ya Viziwi ya huko Magharibi mwa Pennsylvania.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Jankowski, Katherine (2001). "'Til All Barriers Crumble and Fall: Agatha Tiegel's Presentation Day Speech in April 1893.". Katika Bragg, Lois (mhr.). Deaf world : a historical reader and primary sourcebook. New York: New York University Press. ku. 284–295. ISBN 0814798527.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Agatha Tiegel Hanson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |