Admerali
Mandhari
(Elekezwa kutoka Admirali)
Admerali (pia: admeri, admirali) ni cheo cha kiongozi mkuu wa kijeshi wa wanamaji. Cheo hicho kinalingana na jenerali katika matawi mengine ya jeshi.
Neno linatokana na Kiarabu أمير البحر amir-al-bahr yaani "mwenye mamlaka baharini". Iliingia katika lugha za Ulaya kama "admiral".
Cheo hicho si kawaida katika jeshi la majini la Tanzania wala Kenya, lakini hutumiwa kutafsiri vyeo vya kigeni[1].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Linganisha "Admeri", katika Kamusi Kuu ya Kiswahili, Longhorn - Bakita 2016, ISBN 9789987020984