Acetylcysteine
Jina la Utaratibu la (IUPAC) | |
---|---|
(2R)-2-acetamido-3-sulfanylpropanoic acid[1] | |
Data ya kikliniki | |
Majina ya kibiashara | Acetadote, Fluimucil, Mucomyst, mengineyo |
AHFS/Drugs.com | Monograph |
Taarifa za leseni | US Daily Med:link |
Kategoria ya ujauzito | B2(AU) B(US) |
Hali ya kisheria | Pharmacy Only (S2) (AU) OTC (US) |
Njia mbalimbali za matumizi | kwa mdomo, sindano, kwa kuvuta pumzi |
Data ya utendakazi | |
Uingiaji katika mzunguko wa mwili | 10% (kwa mdomo)[2] |
Kufunga kwa protini | 50 hadi 83%[3] |
Kimetaboliki | Ini[3] |
Nusu uhai | Masaa 5.6 [4] |
Utoaji wa uchafu | Figo (30%),[3] kinyesi (3%) |
Vitambulisho | |
Nambari ya ATC | ? |
Visawe | N-acetylcysteine; N-acetyl-L-cysteine; NALC; NAC |
Data ya kikemikali | |
Fomyula | C5H9NO3S |
Massi ya molekuli | 163.195 |
| |
Data ya kimwili | |
Kiwango cha kuyeyuka | 109–110 °C (228–230 °F) [5] |
Spec. rot | +5° (c = 3% ndani ya maji)[5] |
(Hiki ni nini?) (thibitisha) |
Acetylcysteine, pia inajulikana kama N-acetylcysteine (NAC), ni dawa ambayo hutumiwa kutibu kuzidiwa na dozi ya paracetamol (acetaminophen), na kulegeza kamasi nene kwa watu walio na nyuzinyuzi za cystic au ugonjwa sugu wa mapafu.[3] Inaweza kuchukuliwa kwa njia ya mshipa, kwa mdomo, au kwa kuvuta pumzi kama ukungu.[3] Baadhi ya watu huitumia kama virutubisho vya lishe.[6][7]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kichefuchefu na kutapika wakati inachukuliwa kwa mdomo.[3] Ngozi mara kwa mara inaweza kuwa nyekundu na kuwasha kwa namna yoyote ile.[3] Aina isiyo ya kinga ya anaphylaxis inaweza pia kutokea.[3] Inaonekana kuwa salama wakati wa ujauzito.[3] Katika hali ya kuzidiwa na dozi ya paracetamol, inafanya kazi kwa kuongeza kiwango cha glutathione, antioxidant ambayo inaweza kupunguza bidhaa za sumu zinazotokana na mchakato wa kuvunjika kwa paracetamol.[3] Inapovutwa kwa pumzi, hufanya kama mucolytic kwa kupunguza unene wa kamasi.[8]
Acetylcysteine ilipewa hati miliki awali katika mwaka wa 1960 na ikaanza kutumika kimatibabu katika mwaka wa 1968.[9] Iko kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika la Afya Ulimwenguni.[10] Inapatikana kama dawa ya kawaida na ni ya bei nafuu.[11] Mwongozo juu ya matumizi yake hutofautiana kati ya nchi.[11]
Marejeleo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "L-Cysteine, N-acetyl- - Compound Summary". PubChem Compound. USA: National Center for Biotechnology Information. 25 Machi 2005. Identification. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Januari 2014. Iliwekwa mnamo 9 Januari 2012.
- ↑ Stockley, Robert A. (2008). Chronic Obstructive Pulmonary Disease a Practical Guide to Management. Chichester: John Wiley & Sons. uk. 750. ISBN 9780470755280. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Septemba 2017.
- ↑ 3.00 3.01 3.02 3.03 3.04 3.05 3.06 3.07 3.08 3.09 "Acetylcysteine". The American Society of Health-System Pharmacists. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Septemba 2015. Iliwekwa mnamo 22 Ago 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "ACETADOTE (acetylcysteine) injection, solution [Cumberland Pharmaceuticals Inc.]". DailyMed. Cumberland Pharmaceuticals Inc. Juni 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Januari 2014. Iliwekwa mnamo 8 Novemba 2013.
- ↑ 5.0 5.1 "N-ACETYL-L-CYSTEINE Product Information" (PDF). Sigma. Sigma-aldrich. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 11 Juni 2014. Iliwekwa mnamo 9 Novemba 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Talbott, Shawn M. (2012). A Guide to Understanding Dietary Supplements (kwa Kiingereza). Routledge. uk. 469. ISBN 9781136805707. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Septemba 2017.
- ↑ "Cysteine". University of Maryland Medical Center (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Julai 2017. Iliwekwa mnamo 23 Juni 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Sadowska, Anna M; Verbraecken, J; Darquennes, K; De Backer, WA (Desemba 2006). "Role of N-acetylcysteine in the management of COPD". International Journal of Chronic Obstructive Pulmonary Disease. 1 (4): 425–434. doi:10.2147/copd.2006.1.4.425. ISSN 1176-9106. PMC 2707813. PMID 18044098.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unflagged free DOI (link) - ↑ Fischer, János; Ganellin, C. Robin (2006). Analogue-Based Drug Discovery. Weinheim: Wiley-VCH. uk. 544. ISBN 9783527607495. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Septemba 2017.
- ↑ World Health Organization (2019). World Health Organization model list of essential medicines: 21st list 2019. Geneva: World Health Organization. hdl:10665/325771. WHO/MVP/EMP/IAU/2019.06. License: CC BY-NC-SA 3.0 IGO.
- ↑ 11.0 11.1 Hitchings, Andrew; Lonsdale, Dagan; Burrage, Daniel; Baker, Emma (2019). The Top 100 Drugs: Clinical Pharmacology and Practical Prescribing (kwa Kiingereza) (tol. la 2nd). Elsevier. ku. 30–31. ISBN 978-0-7020-7442-4. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Mei 2021. Iliwekwa mnamo 9 Novemba 2021.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)