Nenda kwa yaliyomo

AVG Technologies

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka AVG 9.0)
AVG


AVG Technologies ni kampuni ya kompyuta ya Ucheki ambayo inalinda watu dhidi ya virusi, spyware na aina nyingine ya matishio toka mwaka 1991, na software yake ya AVG imefikisha toleo la 9.0.

Tofauti na version 8 mpaka 8.5 ambayo wakati unapotaka kuingiza kwenye computer ni lazima ufunge vitu unavyofanya kwenye computer yako kama unaangalia tovuti fulani au kama unatumia programu ya word kusoma au kuchapa kitu kwanza ndio ikubali, usipofanya hivyo basi itazifunga yenyewe, unapokuwa unataka kuingiza version 9.0 hutauliza suala la kuzima programu nyingine au vile vitu ulivyokuwa unafanya wakati huo ingawa ni muhimu kufanya hivyo ili unapostart settings ziwe tayari installed.

Pamoja na hiyo inaweza kuzuia computer yako kudownload programu ambazo hazitakiwi hizi ni pamoja na zile zinazokusanya taarifa binafsi za watu bila ya wao wenyewe kujua na kuzifuta moja kwa moja kwa kukupa taarifa ambayo ina popoup kwenye taskbar.

Kitu ambacho hupati kwenye toleo la bure ni firewall ambayo ni kama ukuta wako kuzuia wengine wasiweze kukuona kwenye mitandao ingawa kama unatumia windows basi ina firewall yake ingawa haina ufanisi kama hizi zingine kama unataka firewall nzuri mimi huwa natumia zonealarm pia jua hii imenunuliwa na kampuni moja ya huko Israel sasa watu wa mashariki ya kati wanaiogopa sana wanahisi kwamba labda inatumika dhidi yao ila ni moja ya firewall nzuri zaidi duniani haijawahi kushuka kimasoko toka imeanzishwa.

Pia huwezi kupata msaada wa bure toka kwa AVG wenyewe ingawa kuna sehemu ya forum ambayo unawezakuungana na watumiaji wa AVG wa sehemumbalimbali duniani kubadilishana nao mawazo na maswali na game mode hii ina weza kukusaidia pale unapocheza game kwa njia ya mtandao kukulinda dhidi ya shambulio lolote kwa njia ya games.

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu AVG Technologies kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.