Étoile de Dakar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Étoile de Dakar ("Nyota ya Dakar") walikua kundi la muziki lililoongoza muziki wa senegali mwishoni mwa miaka ya 1970 na mwanzoni mwa miaka ya 1980.

Youssou N'Dour alikua mmoja wa waimbaji katika kumdi Hilo na bendi hiyo ilikua sehemu kubwa ya N'Dour kupata umaarufu mkubwa nchini senegali. Kikundi hicho kilianzishwa mnamo mwaka wa 1978 na Badou Ndiaye na washiriki wengine kadhaa wa Star Band baada ya mzozo na Ibra kasse kiongozi wa Star Band na mmiliki wa klabu ya usiku ya Miami huko Dakar ambapo Star Band ilitumbuiza. The Star Band ilikua ni moja ya bendi ya nyumba za klabu za usiku za Dakar iliyo julikana sana mnamo miaka ya 1960 na 1970.[1]Baada ya Kasse kumfukuza mmoja wa wanachama wa Star Band wanachama wengine wakajitoa kwenye msaada wa wanamuziki, wakaungana na kuunda Étoile de Dakar. Mwimbaji El Hadji Faye ambaye apo hawali aliimba katika Star Band na baadae kujitoa kwasababu hakuelewana na Ibra kasse, aliajiriwa mwanzoni. Baadae mwimbaji Mar Seck kutoka No.1 de Dakar aliletwa kwenye bendi hiyo.

Étoile de Dakar ilikua na nafasi muhimu katika mageuzi ya muziki wa senegali,walisaidia kujumuisha vipengele vya muziki wa jadi wa senegali katika mtindo wa densi maarufu ya ushawishi wa kilatini ambao ulitawala,walisaidia kutengeneza mtindi amabao ulijulikana Kama Mbalax. Kwaharaka wakawa moja ya bendi maarufu[2] ya jiji hilo zilizonufaika na kuanzishwa kwa kaseti nchini senegali. Bendi za awali zilitoa kazi zao kuhusu LPs ambazo zilifanya muziki wao usiwe rahisi kupatikana kwa wakazi wa senegali kuliko Kanda za kaseti. Wimbo wao "Jalo" ulijumuishwa kwenye mkusanyiko wa Island Records sound d'Afrique ambao ulikua mahususi kuleta muziki wa kiafrika maskioni mwa wamagharibi mnamo 1981.[3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Étoile de Dakar kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.