Nenda kwa yaliyomo

Uti wa mgongo : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|right|150px| - Uti wa mgongo katika mwili wa kibinadamu Picha:Gray 111 - Vertebral column-coloured.png|thumbnail|Sehem...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 21:38, 5 Juni 2015

- Uti wa mgongo katika mwili wa kibinadamu
Sehemu za uti wa mgongo

Uti wa mgongo ni jina kwa nguzo ya mifupa ambayo ni kitovu cha kiunzi cha mifupa kwa miili ya vetebrata kama binadamu, mamalia wote na pia wanyama wengine wengi.

Kazi ya uti wa mgongo

Nguzo hii ya uti wa mgongo inashika mifupa yote kwa pamoja kuanzia fuvu hadi mabavu hadi mifupa ya chini inayokutana katika fupanyonga.

Pamoja na kuwa kitovu cha kiunzi cha mifupa uti wa mgongo huwa na kazi ya pili muhimu: inatunza ndani yake [neva] za ugwemgongo zinazofikisha amri za ubongo mwilini. Neva za ugwembongo ni nyeti sana; hivyo uharibifu kwenye uti wa mgongo unaoathiri neva hizi kiasi unaweza kusababisha maumivu makali au hata ulemavu kama neva zinakatika na sehemu za mwili hazipokei tena amri kutoka ubongo.

Sehemu za uti wa mgongo

Uti wa mgongo huangaliwa na matibabu kwa sehemu kuu tano:

  • Uti wa shingoni (ing. cervical, lat. pars cervicalis) : inashika fuvu ya kichwa (nyekundu). Ina pingili 7. Mbili za juu zinaunganisha fuvu na utu wa mgongo.
  • Uti wa kifuani (ing. thorax, lat. pars thoracica): sehemu hii (buluu) inashika mabavu yote mahali pake. Ina pingili 12.
  • Uti wa kiuno (ing. lumbar, lat. pars lumbalis): sehemu hii inaunganisha mwili wa juu na mwili wa chini. Inamwezesha mwandamu kugeuza mwili bila kusogeza miguu. Ina pingili 5 (njano).
  • Uti wa nyonga (ing. sacrum, lat. os sacrum) inashika nyonga. Ni pingili tano ambazo kwa kawaida zimeungana kama mfupa mmoja - (kibichi)
  • Uti wa mkia (ing. coccygeal) - inashika musuli kadhaa (zambarau), ina pingili 3-5.

Marejeo

Viungo vya Nje