Zuhura Yunus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Zuhura Yunus
Amezaliwa 1969
London, Uingereza
Nchi Tanzania
Kazi yake utangazaji

Zuhura Yunus (alizaliwa London, Uingereza, 1969) ni mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu na mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo Tanzania. Ameteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan tarehe 1 Februari 2022. [1][2]

Kabla ya hapo alikuwa mtangazaji wa BBC, idhaa ya Kiswahili, ambaye amekuwa mwanamke wa kwanza kutangaza kipindi cha Dira ya Dunia. [3][4]

Maisha na kazi

Alizaliwa London na wazazi Watanzania[5].

Licha ya kuwa mtangazaji Zuhura Yunus alikuwa na ndoto ya kuwa Daktari, lakini aliachana na ndoto yake hiyo na kujiunga na utangazaji wa redioni mwaka 2000 nchini Tanzania.

Kabla ya kujiunga na BBC mwaka 2008 alifanya kazi ya utangazaji katika vipindi mbalimbali vya redio kama Redio Times FM na Uhuru FM nchini Tanzania.

Mwaka 2002 alifanya kazi ya uandishi wa habari katika gazeti la The Citizen. Mwaka 2008 alijiunga na BBC Swahili akiwa mtangazaji na mtayarishaji wa matangazo. Mwaka 2014 akiwepo bado BBC alihamia kwenye kipindi cha 'Dira ya Dunia' na kua mtangazaji wa kwanza mwanamke wa kipindi hicho.[6]

Akiwa BBC Zuhura ameripoti na kutangaza matukio muhimu kama vile uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2010 na mbio za Marathon za London. Matukio mengine muimu aliyowahi kutangaza ni pamoja na uchaguzi mkuu wa Marekani wa mwaka 2012, kimbunga cha Sandy pamoja na mazishi wa aliyekua raisi wa kwanza wa Afrika ya Kusini baada ya utawala wa kibaguzi, Nelson Mandela, mwaka 2013. Mafanikio yake mengine akiwa BBC ni pamoja na mahojiana na maraisi mbalimbali wakiwemo raisi mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete na raisi wa Uganda, Yoweri Museven. Zuhura pia alitayarisha makala kuhusu MV Liemba, meli iliyotengenezwa na wajerumani wakati wa vita vya kwanza vya dunia na kuendelea kutumika Kigoma Tanzania kwa muda mrefu.[7]

Zuhura ametumikia shirika la utangazaji la BBC kwa miaka 14 na kuacha rekodi ya kua mtangazaji wa kwanza mwanamke kutoka Tanzania kutangaza kipindi cha Focus on Africa mwaka 2019 na mtangazaji wa kwanza wa shirika hilo anayevaa hijabu. [8]

Elimu

Zuhura ana shahada ya kwanza kutoka chuo cha kiislam cha Uganda na shahada ya uzamivu ya mawasiliano kutoka chuo cha Leicester, Uingereza.[9]

Tuzo mbalimbali

Mwaka 2000 alishinda tuzo ya habari ya Ishi nchini Tanzania kutokana na ripoti yake kuhusu virusi vya ukimwi na Ukimwi[10].

Marejeo

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zuhura Yunus kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.