Ziwa Superior

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ziwa Superior pamoja na maziwa makubwa
Desemba 2004

Ziwa Superior (yaani Ziwa Kubwa) ni moja kati ya maziwa makubwa ya Amerika Kaskazini. Ni ziwa kubwa zaidi la bara hili. Pamoja na maziwa ya Ziwa Huron, Ziwa Erie na Ziwa Ontario liko mpakani kati ya Marekani na Kanada na mpaka huo umepita ziwani.

Ziwa limepakana na Kanada (Ontario) upande wa kaskazini halafu na Marekani (Minnesota, Wisconsin na Michigan) upande wa kusini.

Ziwa Superior hupokea maji yake kutoka mito mingi inayoishia humo; maji yake hutoka kwenda Ziwa Huron kupitia mto St. Mary's na Soo Locks.

Vipimo[hariri | hariri chanzo]

Ziwa lina urefu wa kilomita 563 na upana mkubwa wa km 257. Uso wake una eneo la km2 82,400. Kina cha wastani ni m 147 lakini kina kikubwa chafikia m 406.

Maziwa makubwa ya Amerika Kaskazini[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ziwa Superior kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kanada bado ni mbegu.