Voyager 1
Voyager 1 ni chombo cha angani kilichorushwa mwaka 1977 na shirika la NASA nchini Marekani kwa kusudi la kupeleleza anga katika mfumo wa jua letu hadi anga la nje kati ya nyota. Inaendelea kufanya kazi na kutuma data inayokusanya kwa kutumia vyombo vya upimaji ndani yake. Voyager 1 ni chombo cha kutengenezwa na binadamu kilichofikia umbali mkubwa na dunia yaani 123.5 vizio astronomia vinavyolingana na kilomita bilioni 18.35; nuru ya jua inahitaji zadi ya masaa 17 kufikia voyager 1 (hali ya Desemba 2012).
Mwaka 2012 ilitembea nje ya mzingo wa Pluto katika kanda la heliosheath penye mata ya mwisho inayoshikwa na graviti ya jua ikiandaa kuondoka katika mfumo wa jua letu kabisa na kuingia anga kati ya nyota.
Voyager 1 ilipita karibu na sayari za Jupiter na Saturn na kupiga pacha bora za sayari hizi na miezi yao. Inaendelea kupima mnururisho uliopo angani na kutuma data duniani. Inachukua nguvu yake kutoka beteri zenye Plutoni nururifu zinazopangwa kutoa umeme hadi mwaka 2020.
Yaliyomo |
Picha za Mshtarii (Jupiter) zilizotumwa na Voyager 1 [hariri]
-
Doa Kubwa Jekundu katika angahewa ya Mshtarii (Jupiter) jinsi ilivyoonekana kutoka Voyager 1.
-
Picha ya Io mwezi wa Mshtarii.
Saturn [hariri]
Marejeo [hariri]
Viungo vya nje [hariri]
- NASA Voyager website
- Voyager Spacecraft Lifetime — interstellar mission coverage.
- Spacecraft Escaping the Solar System — current positions and diagrams
- CNN: "NASA: Voyager I enters solar system's final frontier", 25 Mei 2005
- CNN: "NASA: Voyager II detects solar system's edge", 25 Mei 2006
- Weekly Mission Reports — includes information on current spacecraft state
