Visa Inc.

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nembo yake.

Visa Inc. (ambayo inajulikana kwa kifupi kama Visa) ni kampuni ya kifedha ya Marekani ambayo inasaidia watu kutoka nchi tofauti kutuma na kupokea pesa kwa njia ya kielektroniki. Kampuni hii huwa na makao yake maalumu jijini Foster, California, kule Amerika. Kampuni ya Visa huwa haitoi kadi za mikopo (credit) au kadi za debit lakini huwezesha benki kuwapa wateja wake huduma za Visa za kutuma na kupokea fedha kwa njia ya kielektroniki.

Mwaka 2015, kampuni ya Nielsen Report ambayo hufanya takwimu za kibiashara walitoa ripoti kuwa Visa iliwezesha shughuli bilioni mia moja kwa huduma zao mwaka 2014 peke yake.

Visa inafanya shughuli zake katika mabara yote isipokuwa Antaktika. Vituo vya data vya Visa viko Ashburn, Virginia, Highlands Ranch, Colorado, London na Singapore. Vituo hivi huwa vimelindwa dhidi ya wizi na ugaidi.

Historia ya Visa Inc.[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Septemba 1958, benki ya Amerika ilianzisha kadi yake ya mikopo BankAmericard ikaweza kutoa kadi elfu sitini kwa wateja wake. Shughuli hii iliweza kufana na kutolewa nakala na Barclaycard, CarteBleue, Chargex na Sumitomo card. Mwaka 1976, makampuni hayo yote yalishirikiana na kuona heri wawe pamoja na kujiita Visa, huduma itakayoweza kuwafikia watu wa mabara yote.

Jina Visa lilibuniwa na mwanzilishi Dee Hock ambaye alisema kuwa jina hili ni jepesi kukumbukwa na litaweza kuonekana na watu wa mabara yote kama jina la kadi ambayo yaitikiwa kote.

Sifa ya kadi za Visa[hariri | hariri chanzo]

Kwa kawaida, kadi ya Visa huwa na nambari ya kadi (BIN number list) ambayo ni ya pekee kwa kila mteja na hujulikana na yafaa mteja aiweke kwa siri isijulikane. Pia huwa na nambari ya CSV au CVV ambayo ni nambari tatu zilizoko nyuma ya kadi. Nambari hii huzuia wizi na anayetumia kadi kufanya shughuli za ununuzi kwa mitandao hufaa aiweke ili ikubaliwe.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Visa Inc. kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.