Tunguska
Tunguska ni eneo kubwa katika Siberia kati ya mito miwili inayoitwa Tunguska ya mawe na Tunguska ya chini ambalo liko katika kusini-mashariki ya mkoa Krasnoyarsk Krai wa Urusi. Ni eneo lisilokaliwa na watu wengi.
Yaliyomo |
Tukio la Tunguska [hariri]
Mwaka 1908 mlipuko mkubwa ulitokea juu ya eneo la Tunguska unaoaminiwa kusababishwa na gimba kubwa kutoka anga la nje kama kimondo kikubwa au asteroidi ndogo lililoingia katika angahewa na kupasuka kilomita kadhaa juu ya Tunguska.
Mashahidi walitoa taarifa juu ya mlio mkubwa kama mfululizo wa milipuko au mapigo ya mabunduki kwa mbali mnamo saa 7.15 asubuhi tarehe 30 Juni 1908 (tar. 17 Juni katika kalenda ya Juliasi). Watu wachache walisimulia ya kwamba walisikia milipuko mbalimbali. Katika eneo kubwa miti iliangushwa. Milango na madirisha ya nyumba katika kijiji cha Vanavara kilichokuwa na umbali wa kilomita 65 kutoka eneo la mlipuko ilivunjika.
Kwa umbali wa kilomita 500 wako wa nuru na tetemeko zilitazamiwa na abiria kwenye reli ya Siberia.
Hakuna uhakika kama watu walikufa kwa sababu wakazi wa pekee katika eneo hili walikuwa wavindaji wa kabila la Waevenki.
Taarifa ya kwanza la eneo lenyewe linapatikana kutokana msafara wa mwanasayansi Mrusi Leonid Kulik aliyekaribia Tunguska mwaka 1922; 1927 alifika hadi kiini cha uharibifu na 1938 picha zilipigwa kutoka eropleni. Alikuta ya kwamba miti ilianguka katika kanda ya upana wa 70 km na urefu wa 55 km jumla eneo la 2,150 km². Kitovu chake kilikuwa kanda la kilomita 8 lenye miti iliyochomwa na bila matawi ilhali ilisimama.
Hakuna kasoko lililotazamiwa na wataalamu wakati ule.
Maelezo mbalimbali [hariri]
Leonid Kulik alikuwa mtaalamu wa kwanza aliyehisi ya kwamba uharibifu ilisaabishwa na mshtuko kutokana na kimondo kilichoingia katika angahewa ya dunia na kupashwa joto hali halafu kupasuka kilomita kadhaa juu ya uso wa ardhi.
Hadi leo wataalamu wengi wanakubali elezo hili ingawa kuna majadiliano kama gimba la Tunguska lilikuwa kimondo, nyotamkia au asteroidi. Tatizo la maelezo yote ni ukosefu wa vipande vinavyotazamiwa kuwa na asili ya kimondo. Kinyume chake nyotamkia kubwa inaweza kueleza kutokuwepo kwa vipande kwa sababu inafanywa na barafu na vumbi tu lakini wengi hawaamini ya kwamba ingeweza kufikia karibu na uso wa ardhi vile bila kuyeyuka tayari katika kimo kikubwa.
Mwaka 2007 wanasayansi kutoka Italia walichungulia ziwa lililopo katika Tunguska wakaamini ya kwamba ziwa hili linajaza kasoko lililosababishwa na kipande cha gimba la Tunguska ingawa wataalamu wengine wana mashaka.
Wanasayansi wachache Warusi na Wajerumani waliunda nadharia ya kwamba sababu ya uharibufu ilikuwa tukio kutoka ndani ya ardhi ambako akiba kubwa ya gesi asilia ndani ya ganda la ardhi lilipasuka na kutoka ghafla hewani ilipowaka kilomita kadhaa juu ya ardhi.
Tunguska kama mfano wa hatari kutoka anga la nje [hariri]
Wataalamu wengi wanaotazama gimba la Tunguska kama gimba la angani wanatumia uharibifu uliosababishwa nalo kama mfano wa hatari kutoka anga la nje. Tunguska haikupata vifo vingi vya wanadamu mwaka 1908 kwa sababu ilikuwa eneo tupu bila makazi ya watu. Lakini kama gimba la Tunguska lingeanguka juu ya mji mkubwa idadi ya wafu ingeweza kufikia malakhi au hata mamilioni ya watu. Tena astronomia imegundua ya kwamba kuna magimba mengi na makubwa zaidi yanayozunguka katika mfumo wa jua letu. Inajulikana ya kwamba yale magimba makubwa yanaweza kuvutwa na graviti ya dunia na kuanguka hapa. Kasoko kubwa sana zimetazamiwa duniani na pia kwenye sayari nyingine zilizosababishwa na mapigo ya vimondo na asteroidi. Sayansi imekadiria ya kwamba nishati ya mapigo yaliyosababsha kutokea kwa kasoko hizi kubwa inapita nguvu ya mabomu makubwa ya kinyuklia.
Hapa mataifa ya dunia yameanza majadilian juu ya ushirikiano kutambua magimba ya angani yanayolenga dunia yetu na kuandaa mbinu za kuzizuia kwa mfano kwa kupeleka mabomu katika anga la nje na kuyapasua mbali na dunia au kuyalenga upande mwingine.
Vitabu [hariri]
- Andrei E. Zlobin Quasi Three-dimensional Modeling of Tunguska Comet Impact (1908) (2007) paper in 2007 Planetary Defense Conference
Viungo vya Nje [hariri]
- The Tunguska Event in 1908: Evidence from Tree-Ring Anatomy - Astrobiology, Volume 4, Number 3, 2004, pp. 391–399
- (Kiingereza) Makala ya Chyba, Zahnle na Thomas ya 1993 katika jarida ya kisayansi Nature
- (Kiingereza) Hipothesi ya mlipuko wa volkeno na A. Ol'khovatov
- (Kiingereza) Tunguska: mlipuko chini ya ardhi?
- (Kiingereza) Kuhusu swali la kasoko katika Tunguska, Sky & Telescope, 22 Juni 2007.
- (Kiingereza) The Carolina Bays
- (Kiingereza) Large Aerial Bursts: An Important Class of Terrestrial Accretionary Events
- (Kiingereza) Tunguska
- (Kiingereza) Tunguska genetic anomaly and electrophonic meteors
- (Kiingereza) Tunguska isn't a mystery any more!
