Teresia Mbari Hinga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Teresia Mbari Hinga ni mwanateolojia Mkristo mpaniaji wa haki za wanawake kutoka nchini Kenya, ambaye ni profesa wa elimu ya dini katika chuo kikuu cha Santa Clara huko California.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Hinga alizaliwa Kenya. Mama yake akijulikana kama Agnes Wairimu na baba kama Ernest Hinga, ambao walikuwa Waanzilishi wa masuala ya Ukatoliki Afrika, ambao waliwalea watoto wao wote wa kiume na wa kike kwa usawa bila ubaguzi wala upendeleo, ikiwemo kuwapatia elimu[1]. Hinga alipelekwa kwenye shule ya sekondari ya Loreto[2]. Alitunukiwa shahada ya uzamivu (digrii) katika masuala ya fasihi za kiingereza na masomo ya dini kutoka chuo kikuu cha Kenyatta 1977 na pia shahada ya uzamili katika masomo ya dini kutoka chuo kikuu cha Nairobi mnamo 1980.[3]

Pia alitunukiwa shahada ya PhD kutoka chuo kikuu cha Lancaster huko Uingereza mnamo 1990 kupitia kichwa cha tafiti kisemacho Women, Power and Liberation in an African Church: A Theological Case Study of the Legio Maria Church kikiangalia maisha ya wanawake Wakristo wa nchini Kenya.[4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "WATERtalk Notes with Teresia Mbari Hinga – WATER – Women's Alliance for Theology, Ethics and Ritual" (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2022-02-17. 
  2. Teresia, Hinga (2017-12-14). African, Christian , Feminist: The Enduring Search For What Matters (kwa Kiingereza). Orbis Books. ISBN 978-1-60833-714-9. 
  3. "Teresia Hinga - College of Arts and Sciences - Santa Clara University". www.scu.edu. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-02-17. Iliwekwa mnamo 2022-02-17. 
  4. Hinga, Teresia Mbari (1990). Women, Power and Liberation in an African Church: A Theological Case Study of the Legio Maria Church in Kenya (kwa Kiingereza). University of Lancaster.