Slobodan Milosevic

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Milošević mwaka wa 1996

Slobodan Milosevic (20 Agosti, 1941 - 11 Machi, 2006) alikuwa Rais wa Serbia kuanzia mwaka 1989 hadi 2000. Pia alikuwa rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Yugoslavia kutoka 1997 hadi 2000. Aliongoza Chama cha Kijamaa cha Serbia kutoka msingi wake mnamo 1990 na aliibuka na kuwa Rais wa Serbia wakati ambao juhudi za kurekebisha Katiba ya Yugoslavia ya mwaka 1974 zilikuwa zikianza. Katiba hiyo ilikuwa haina uwezo wa kisiasa kuzuia mizozo katika Albania na jimbo la Kosovo la Serbia yaliyokuwa yakitaka kujitenga tangu awali.

Asili ya Milosevic ilianzia katika kijiji cha Lijeva Rijeka pale Podgorica na ukoo kutoka Montenegro. Alizaliwa Požarevac, mji ambao upo kati ya mito mitatu ya Danube, Great Morava na Mlava. Milosevic alizaliwa miezi minne baada ya uvamizi wa Falme ya Yugoslavia uliofanywa na mataifa Ujerumani, Italia na Japan yalikuwa yakifahamika kama Roberto. Milosevic alikuwa na kaka yake ambaye baadaye alikuja kuwa Mwanadiplomasia. Baba yake Milosevic alijiua mwaka 1962.

Pia mama yake aliyekuwa akifahamika kwa jina la Stanislava ambaye alikuwa mwalimu wa shule na mwanachama hai wa Chama cha Kijamaa alijiua mwaka 1972. Milosevic alisoma sheria katika Chuo Kikuu cha Belgrade.

Milosevic anakumbukwa kutokana na kuwa chanzo cha anguko la Shirikisho la kijamaa la Jamhuri ya watu wa Yugoslavia mwanasiasa huyu wa Serbia mwenye msimamo mkali aliingia madarakani kupitia harakati kali za utaifa wa Serbia, baada ya kushika hatamu ya madaraka ya rais wa urais wa Jamhuri ya kijamaa ya Serbia mnamo Mei 8, 1989 hadi Januari 11 1991 na Urais wa Jamhuri ya Serbia kuanzia Januari 11, 1991– Julai 23 1997.

Kitendo chake cha kutaka kuwapa nguvu kubwa raia wachache wenye asili ya Serbia ambao ni Wakristo katika jimbo la Kosovo dhidi ya raia wenye asili ya Albania walio wengi na ambao pia ni Waislamu kwa madai kuwa raia wenye asili ya Serbia ambao ni Wakristo walikuwa wanabaguliwa katika jimbo hilo. Pia hatua yake ya kupingana na jamhuri nyingine zilizokuwa zinaunda shirikisho la kijamaa la Yugoslavia katika mpango wa kulifanyia mageuzi shirikisho hilo kulipelekea kuibuka kwa chuki kali dhidi ya raia wenye asili ya Serbia waliokuwa wakiishi katika Jamhuri nyingine za shirikisho.

Akiungwa mkono na wanaharakati wa utaifa wa Serbia walio wachache kutoka Kosovo na Bosnia-Herzegovina pia kwa kupewa msaada na washirika wake katika television ya Taifa ya Serbia, aliendelea kueneza chuki miongoni wa raia wenye asili ya Serbia walio wachache katika jamhuri za Croatia na Bosnia. Television ya Serbia ilikuwa ikionyesha matukio ya mauaji ya kutisha yaliyofanywa na mafashisti wa Croatia dhidi ya Waserb wakati wa vita kuu ya pili ya Dunia.

Hofu ilitawala miongoni mwa jamii ya Waserb huko Croatia na Bosnia kwamba hatima kama hiyo iliyowakuta wenzao na wao inawasubiri. Hali hii ilipelekea kuibuka kwa itikadi za kuweka msingi wa uanzishwaji wa Serbia kubwa "Greater Serbia" taifa ambalo halitakuwa Serbia tu, bali litakalojumuisha na maeneo ya Bosnia na Croatia yenye idadi kubwa ya wakazi wenye asili ya Serbia.

Na ili kufanikisha mpango huo, mkakati uliokuwa umewekwa ilikuwa ni kuwaondoa raia wote wasiokuwa Waserb ( Ethnic Cleansing) katika Serbia na miji inayokaliwa na Waserb wengi katika jamhuri za Croatia na Bosnia. Mnamo Machi 26, 1990 uongozi wa Serbia chini ya Rais Slobadan Milosevic ulikutana kujadili hali ya uhasama ulivyokuwa ikiendelea ndani ya shirikisho la Yugoslavia na kufikia makubaliano rasmi kuwa vita katika Jamhuri za Croatia na Bosnia-Herzegovina ni suala lisiloepukika. Mnamo Julai 2, 1990 bunge la Kosovo nalo lilitangaza kuwa Kosovo ni Jamhuri yenye hadhi kama zilivyo jamhuri nyingine sita zilizokuwa zikiunda shirikisho la Yugoslavia. Kufuatia tangazo hilo, Bunge la Serbia lilipiga kura kuweka marufuku kwa jimbo la Kosovo lenye Waislamu wengi ambao ni wakazi wenye asili ya Albania kuwa na Bunge lake.

Milosevic alifariki dunia Machi 11, 2006. Milošević alikutwa amekufa katika seli yake ya gereza katika Mahakama ya Uhalifu wa Kivita ya ICC, The Hague, Uholanzi.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Slobodan Milosevic kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.