Sheila Tlou

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Profesa Sheila Dinotshe Tlou ni muuguzi, mtaalamu wa VVU / UKIMWI na afya ya wanawake, na mwalimu wa uuguzi wa Botswana. Alikuwa Waziri wa Afya kutoka mwaka 2004 hadi 2008.[1] Profesa Tlou ametambuliwa kama kiongozi katika masuala ya afya akikazia hasa maswala ya kuboresha elimu na mazingira ya kazi ya wauguzi na matibabu.[2]

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Alikulia nchini Botswana, alisoma shule iliyofundishwa na watawa wa Kiayalandi; alikuwa na kipawa cha lugha na mchezo wa kuigiza, ambayo ilimpa motisha katika ndoto yake ya kufanya kazi Hollywood.[3] Tlou alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Dillard mnamo mwaka 1974.

Mnamo mwaka 2014 alipewa tuzo ya Shahada ya heshima na Chuo alichosomea.[4] Tlou alisoma katika Chuo cha Ualimu, Chuo Kikuu cha Columbia, U.S., akipata MA katika Elimu (akizingatia Mtaala na Mafundisho katika Sayansi ya Afya).[5] Alihitimu PhD yake katika fani ya uuguzi wa afya ya jamii na astashahada katika maswala ya kijinsia, katika Chuo Kikuu kilichopo Illinois huko Chicago mnamo 1990.[6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nurse leader heads health ministry in Botswana". International Nursing Review (kwa Kiingereza) 52 (1): 10–11. 2005. ISSN 1466-7657. doi:10.1111/j.1466-7657.2004.00412_5.x. 
  2. "WHO | Alliance Champion Professor Sheila Tlou". WHO. Iliwekwa mnamo 2021-08-08. 
  3. "UIC Nursing alum one of '100 Most Influential African Women' | College of Nursing | University of Illinois Chicago". nursing.uic.edu. Iliwekwa mnamo 2021-08-08. 
  4. dualumni (2014-05-30). "Dillard University Bestowed Honorary Degrees to Dr. Henry Lacey & Dr. Sheila Tlou". DU ALUMNI NEWS (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-08. 
  5. "Dr Sheila Tlou, Director, UNAIDS Regional Support Team for East and Southern Africa". web.archive.org. 2011-12-07. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-12-07. Iliwekwa mnamo 2021-08-08. 
  6. "W.K. Kellogg Foundation: African KILP Fellows - Programming". web.archive.org. 2007-09-27. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-27. Iliwekwa mnamo 2021-08-08. 
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sheila Tlou kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.