Rachid Belhout

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Rachid Belhout (14 Juni 1944 - 9 Agosti 2020) alikuwa meneja na mchezaji wa kandanda wa Algeria. Wakati wa kifo chake, alikuwa akisimamia klabu ya Al-Ahly Benghazi katika Ligi Kuu ya Libya.

Binafsi[hariri | hariri chanzo]

Belhout alizaliwa mnamo Juni 14, 1944 huko Sétif. Akiwa na umri wa miaka 4, alihamia Ufaransa pamoja na familia yake.[1]

Usimamizi Katika Kazi[hariri | hariri chanzo]

Belhout alipokea leseni yake ya ukocha kutoka Shirikisho la Soka la falme za Ubelgiji.[2] Alianza kazi yake kwa kufundisha timu kadhaa za vijana ligi za professional huko Ubelgiji na Luxemburg.

Kifo[hariri | hariri chanzo]

Belhout alifariki 9 Agosti 2020, akiwa na umri wa miaka 76, baada ya kuhusika katika mgongano wa trafiki huko Nancy, Ufaransa.[3]

Heshima[hariri | hariri chanzo]

Meneja

  • Alishinda Kombe la Rais wa Tunisia mara moja akiwa na klabu ya Olympique Béja mnamo 2010
  • Alishinda Kombe la Algeria mara moja akiwa na klabu ya JS Kabylie mnamo 2011
  • Mshindi wa Fainali ya Kombe la Algeria mara moja akiwa na klabu ya USM Alger mnamo 2007

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo Vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rachid Belhout kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.