Nyumba ya Utopia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nyumba ya Utopia (kwa Kiingereza: Utopia House) ni nyumba ya makumbusho ya kihistoria yanayopatikana katika jiji la Zimbabwe yakiwa ni jumba la kwanza la kisasa kujengwa mwaka 1897.

Hapo awali ilikuwa nyumba ya Rhys Fairbridge, mmoja wa walowezi Wazungu wa mapema katika eneo hilo. Vitu vya ndani ya nyumba hiyo vina muonekano wa miaka ya 1910, zikiwemo samani za ndani ambazo zilikuwa zikitumiwa na Rhys, Utopia ni moja kati ya majumba mawili ya makumbusho yanayopatikana katika jiji la Mutare.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Nyumba ya Utopia ilijengwa mwaka 1897 kama makazi ya Rhys na Rosalie Fairbridge, Rhys Fairbridge aliwasili Manicaland mapema katika miaka ya 1890 kwa ajili ya kazi za utafiti chini ya kampuni ya Uingereza. Alichunguza ardhi ya Mutare na maeneo ya jirani. Alijenga nyumba kwa ajili yake na mke wake.

Utopia ilikuwa ni moja ya nyumba nzuri zilizojengwa kwa ajili yake wakati akifanya uchunguzi. Hii ilikuwa nyumba ya kwanza kujengwa kwa mawe ikiwa na ukuta mrefu ila kwa bahati mbaya ujenzi wake ulisimama kwa sababu ya matatizo ya kifedha na muingiliano wa hali ya hewa na mvua. Katika kuta ambazo zilikuwa hazijakamilika alijenga kwa miti ya mianzi na vitu vya asili vilivyokuwa vikipatikana katika eneo hilo. Ilikuwa nyumba ya kwanza kuwa na muonekano wa mtindo wa nyumba za Ulaya katika jiji la Mutare.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Figure 3: The first modern house to be built in Mutare in 1897, Utopia...". ResearchGate (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-11-28. 
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyumba ya Utopia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.