Nembo ya Kenya
Mandhari
Nembo ya Kenya huonyesha simba wawili wanaoshika mishale na ngao ya Maasai. Ngao huoneyesha rangi za taifa zilizogawanyika katika sehemu nne.
- Nyeusi humaanisha watu wazaliwa Kenya
- Kijani humaanisha kilimo na maliasili
- Nyekundu humaanisha mapambano kupata uhuru
- Nyeupe humaanisha umoja na usalama
Sehemu nyekundu huonyesha jogoo anayeshika shoka; hii humaanisha maisha bora. Ngao na simba wamesimama juu ya Mlima Kenya. Chini ya ngao kimeandikwa Harambee.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]http://www.kenyarchives.go.ke/emblem.htm Ilihifadhiwa 8 Mei 2006 kwenye Wayback Machine.