Mapinduzi ya kijeshi ya 1982 nchini Kenya
Mapinduzi ya kijeshi ya 1982 nchini Kenya ilikuwa jaribio lililoshindikana la kumpindua rais Daniel arap Moi.
Yaliyomo |
[hariri] Matokeo ya 1982
Jumamosi tar. 1 Agosti 1982 kundi la wanajeshi wa anga walivamia kituo cha redio ya Sauti ya Kenya wakidai kuwa wamepindua serikali. Kiongozi wao alikuwa Hezekiah Ochuka afisa wa ngazi ya chini akishirikiana na wenzake. Tangazo lao lilikuwa: "Serikali ya Kenya imepinduliwa na majeshi na sasa iko mikononi mwa majeshi. Viongozi wetu wamekuwa watu wafisadi wenye matumbo makubwa wasiojali maskini."
Tanganzo lilisababisha watu wengi kuanfdamana mjini na kupora maduka wakilenga hasa raia wa asili ya Kihindi mjini Nairobi. Imekadiriwa ya kwamba zaidi ya maduka 1,000 yaliporwa na nyumba za Wahindi zilivunjwa na wanawake wao kunajisiwa.
[hariri] Jeshi la ardhi na polisi wakandamiza uasi
Jaribio la mapinduzi halikudumu muda mrefu baada ya jeshi la ardhi pamoja na polisi kuingia kati na kukandamiza uasi baada ya masaa sita tu. Rais Moi alikuwa nje ya Nairobi na mipango ya kurusha mabomu kwa nyumba yake huko Kabarnak haikutekelezwa.
Hezekia Ochuka alikamata ndege akakimbilia Tanzania alipokamatwa na kurudishwa Kenya baadaye alipopelekwa mahakamani na kunyongwa baadaye kama msaliti.
[hariri] Sababu za uasi
Idadi kubwa ya viongozi wa uasi walikuwa wanajeshi kutoka kabila la Waluo. Inaonekana ya kwamba jaribio lilisababishwa na azimio la Bunge la Kenya la tar. 9 Juni 1982 lililofanya Kenya kuwa nchi ya chama kimoja. Sheria hii ilizuia jaribio la kiongozi wa Kiluo Jaramogi Oginga Odinga kuanzisha chama cha upinzani.
[hariri] Yaliyofuata
Uasi ulisababisha ukandamizi mkali. Polisi ilipita katika nyumba za askari wa anga pia katika mitaa ya vibanda ambako amelfu walikamatwa. Jeshi la anga lilifutwa. Jumla la watu 145 waliuawa ama na waasi au baadye katika ukandamizi wake.
Viongozi wa Waluo walikamatwa pia; Jaramogi Odinga alifungwa katika nyumba yake na kushtakiwa lakini mashatki yaliondolewa baadaye lakini mwanake Raila Odinga alifungwa jela kwa miaka sita hata bila kuhukumiwa.
Kwa jumla siasa ya rais Moi ilibadilika kuwa ya kidikteta baadaye na polisi ilipewa mamlaka pana kutafuta wapinzani kata kuwatesa na kuwakamata bila kuwapeleka mahakamani.