Nenda kwa yaliyomo

Muharram

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Muharram (mwezi))

Muharram (kwa Kiarabu: محرم ) ni mwezi wa kwanza katika kalenda ya Kiislamu. Ni kati ya miezi minne mitakatifu ya mwaka.

Jina la mwezi limetokana na neno "haram" yaani "mwiko" au "kukatazwa" kwa maana ya kwamba vita haitakiwi mwezi huo.

Siku ya kwanza ya Muharram ni Mwaka Mpya wa Kiislamu.

Sikukuu ya Ashura iko tarehe 10 Muharram. Hasa Waislamu Washia hukumbuka kifo cha Hussein ibn Ali (mjukuu wa Mtume Muhammad anayeheshimiwa kama Imamu wa Washia) kwenye mapigano ya Kerbela.

Kwa jumla Washia wanaangalia Muharram kama mwezi wa huzuni na katika mazingira yenye Washia wengi kuna mikutano mingi ya kidini ambako historia ya Ashura na kifo cha Hussein inakumbukwa kuanzia siku ya kwanza hadi ya kumi ambayo ni Ashura.

Kati ya Wasunni siku ya Ashura inatazamwa kama siku ya saumu hasa.[1].

  1. Fadhila Za Mwezi Wa Al-Muharram, Siku Ya 'Aashuraa Na Bid'ah Zake, mkusanyo wa hadith kuhusu saumu ya Muharram, tovuti ya Kisunni ya alhidaaya.com, iliangaliwa Setemba 2018