Michael Rainey Jr.

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Michael Rainey Jr.
Amezaliwa22 Septemba 2000
Majina mengineTariq St. Patrick
Kazi yakeMwigizaji
Miaka ya kazi2010-hadi sasa

Michael Rainey Jr. (anayejulikana sana kwa jina la Tariq St. Patrick kwenye muendelezo wa maigizo ya televisheni ya Power na Power Book II: Ghost; amezaliwa Septemba 22, 2000) ni mwigizaji wa filamu kutoka Marekani.[1]

Maisha ya awali na elimu[hariri | hariri chanzo]

Rainey Jr. alizaliwa huko Louisville, Kentucky, Baba yake anaitwa Michael Rainey Sr. na mama yake ni Shauna Small. Kupitia mama yake ana asili ya Jamaika. Baba yake anatokea New York huku Rainey Jr. akilelewa Staten Island, New York tangu alipokuwa na umri wa mwaka 1. Rainey Jr. ni mshirika wa Find and Feed, shirika lenye makao yake Indiana linalowajali wasio na makazi.[2]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Rainey Jr. alianza kuigiza akiwa na umri wa miaka kumi aliposhirikishwa katika filamu ya Un Altro Mundo na aliendelea kuonekana katika filamu na maigizo ya televisheni mbalimbali kama vile Orange is the New Black, Barbershop, Amateur, 211 na Power.[3]

Rainey Jr. kwa sasa anaigiza kama Tariq St. Patrick kwenye mfuluzizo wa filamu ya Power na Power Books II: Ghost akicheza kama muhusika mkuu.[4]

Filamu[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Filamu Wadhifa
2010 Un Altro Mondo Charlie
2010 Waiting Room Mtoto
2010 Sunny & Share Love You Jason
2012 LUV
2013 The Butler Cecil Gaines
2014 Second Chance Christmas Lawrence
2016 Barbershop: The Next Cut Jalen
2018 Amateur Terron Forte
2018 211 Kenny Rastell

Maigizo ya Televisheni[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Jina la Igizo Wadhifa
2020-hadi sasa Book II Tariq St. Patrick
2014–2020 Power Tariq St. Patrick
2010–2015 Orange Is the New Black Michael Burset

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Michael Rainey Jr. Kwenye IMDb

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Power Book II: Ghost star Michael Rainey Jr reacts to fandom's surprise turnaround". Digital Spy (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-11-27. 
  2. "Michael Rainey Jr.'s bio: age, height, parents, net worth". Legit (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-02-11. 
  3. "Trailer Watch: Ryan Koo’s Amateur worth". Film Maker Magazine (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-03-19. 
  4. "‘Power Book II: Ghost’: David Walton, Monique Curnen & Moriah Brown Join Starz’s Spinoff As Series Regulars". Deadline (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-01-13. 
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Michael Rainey Jr. kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.