Matt Damon
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Matt Damon | |
|---|---|
Matt Damon |
|
| Amezaliwa | Matthew Paige Damon 8 Oktoba 1970 Cambridge, Massachusetts Marekani |
| Kazi yake | Mwigizaji Mwandikaji muswaada andishi Mtayarishaji |
| Miaka ya kazi | 1988–hadi leo |
| Ndoa | Luciana Bozán Barroso (2005–hadi leo) |
Matthew Paige Damon (amezaliwa tar. 8 Oktoba, 1970) ni mwigizaji wa filamu na mhisani kutoka nchini Marekani. Ameshinda Tuzo ya Akademi akiwa kama mwandishi bora muswaada andishi kwa filamu ya Good Will Hunting, ana tunukiwa unyota bora kwa filamu hiyohiyo.
Umaarufu wake ulianza kukua katika soko la filamu kuanzia mwaka wa 1997, tangu hapo akawa ana pambanishwa na waigizaji wakubwa-wakubwa wa wa A-list, na leo hii ni mmoja kati ya waigizaji wakubwa kabisa katika Hollywood.
Damon amepata kushiriki katika baadhi ya filamu maarufu kama vile Saving Private Ryan, The Talented Mr. Ripley, mfululizo wa Ocean, mfululizo wa Bourne, Syriana, The Good Shepherd na The Departed. Amejishindia Matuzo kedekede kwa umahili wake wa uigziaji wa filamu na amepokea nyota katika Hollywood Walk of Fame.
Damon ni mmoja kati ya wale waigizaji ishirini na tano bora kwa muda wote. Katika mwaka wa 2007, alipewa jina na gazeti la People kuwa yeye ni Mwanaume Mwenye Mvuto Aliye Hai.
Damon amekuwa akijishughulisha na kazi za kihisani mara kwa mara, kazi hizo ni pamoja na lujitolea kwa ONE Campaign na H2O Africa Foundation. Pamoja akiwa na mke wake, Bi. Luciana Bozán Barroso, Damon amepata watoto wawili wa kike, mmoja anaitwa Isabella na mwingine anaitwa Gia, na pia ana mtoto wa kufkia Alexa kutoka katika ndoa ya awali aliyofunga Bi. Barroso.
[hariri] Viungo vya nje
- Matt Damon katika Internet Movie Database
- Matt Damon on Moviefone
- Matt Damon News Column
- Matt Damon interview
- Matt Damon on Hardball
- GreenDimes Matt Damon, board member
- Not On Our Watch: George Clooney, Brad Pitt, Matt Damon, Don Cheadle, Jerry Weintraub
| Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani wa Marekani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Matt Damon kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |