Maghrib
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maghrib (المغرب العربي al-maġrib al-ʿarabī; pia: Maghreb) ni sehemu ya kaskazini-magharibi ya Afrika. Siku hizi neno lataja nchi za Moroko, Algeria na Tunisia, wakati mwingine pia Mauretania.
Zamani "Maghrib" ilimaanisha pekee maeneo kati ya pwani la Bahari Mediteranea na vilele vya Milima ya Atlas pamoja na sehemu za Rasi ya Iberia (Hispania, Ureno kusini), Malta na Sisilia zilizotawaliwa na Waislamu.
Viungo vya Nje [hariri]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: