Luteni Kanali
Luteni Kanali (kwa Kiingereza: lieutenant colonel) ni cheo cha afisa wa jeshi, kilicho chini ya Kanali na juu ya Meja.
Asili ya neno luteni ni Kifaransa "lieu-tenant" (yaani "mwenye kushika nafasi") kwa maana ya naibu, makamu. Kiasili lieu-tenant alikuwa makamu wa kapteni, yaani mkuu wa kikosi aliyeshika mamlaka yake wakati hayuko.
Maana hiyo ni pia asili ya vyeo vya Luteni Kanali au Luteni Jenerali vilivyotaja manaibu wa kanali au jenerali.
Baadaye ziliendelea kuwa vyeo vya pekee bila kuunganishwa na nafasi ya makamu tena.
Majeshi ya Afrika yalirithi cheo hicho sawa na vyeo vya kijeshi kwa jumla kutoka mapokeo ya jeshi la kikoloni.
Vyeo vya kijeshi - Tanzania | ||
---|---|---|
Jenerali * Luteni Jenerali * Meja Jenerali * Brigedia * Kanali * Luteni Kanali * Meja * Kapteni * Luteni * Luteni-usu Afisa Mteule Daraja la Kwanza * Afisa Mteule Daraja la Pili * Sajinitaji * Sajenti * Koplo * Koplo-usu |
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |