Kapteni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alama kwenye sare ya kapteni katika jeshi la Tanzania

Kapteni ni cheo cha kijeshi katika nchi nyingi za dunia. Kapteni huwa ni kiongozi wa kikosi cha askari 100-200.

Madaraka ya kapteni ni kuongoza kikosi chake akisaidiwa na maluteni wake. Kwa kawaida hatashiriki katika mipango ya vita bali wajibu wake ni kutekeleza maagizo ya wakubwa wake.

Katika jeshi la wanamaji kapteni (captain) hutokea kama cheo cha kiongozi wa manowari kwa hiyo kuna uwezekano ya kwamba kapteni huyu ana madaraka zaidi kuliko kapteni kwenye nchi kavu.

Neno limeingia katika Kiswahili kutoka lugha ya Kiingereza. Asili ya cheo ni neno la Kilatini "caput" linalomaanisha "kichwa, mkubwa, kiongozi wa kundi".



Vyeo vya kijeshi - Tanzania

Jenerali * Luteni Jenerali * Meja Jenerali * Brigedia * Kanali * Luteni Kanali * Meja * Kapteni * Luteni * Luteni-usu

Afisa Mteule Daraja la Kwanza * Afisa Mteule Daraja la Pili * Sajinitaji * Sajenti * Koplo * Koplo-usu