Lev Yashin

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lev Yashin mwaka 1966

Lev Ivanovich Yashin (22 Oktoba 1929 - 20 Machi 1990) maarufu kama "Black spider" au "Black Panther" alikuwa golikipa kutoka nchini Urusi,wachambuzi wengi wa soka wamesema kwamba huyo ndiye golikipa bora kwa mchezo wa soka kwa kutumia mbinu zake za kuwatisha washambuliaji akiwa golini na kuruka sarakasi akiwa anaokoa mipira,na pia alikuwa mwenyekiti msaidizi wa shirikisho la mpira wa miguu Soviet.

Yashin awapo golini huimarisha safu yake ya ulinzi kwa kuwafokea mabeki wake,alitoka kwenye eneo lake kwenda kuzuia mashambulizi.Alivaa mavazi meusi kuanzia kichwani mpaka miguuni ndiyo maana wakamuita "Black spider" ndiyo sababu ya umaarufu wake.

Yashin alicheza kombe la dunia mara nne kutoka 1958 mpaka 1970 na mwaka 1998 alichaguliwa kwenye timu ya dunia,FIFA inasema kwamba Yashin aliokoa penati 150 kwenye historia ya soka na hakuna golikipa aliyeweza kufanya hivyo na alipokea tuzo ya Ballon d'or na ni golikipa pekee aliyeshinda tuzo hiyo.Mwaka alichaguliwa kuwa golikipa pekee duniani.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lev Yashin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.