Lava

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Lava ni mwamba katika hali ya kiowevu kutokana na joto kali. Chini ya uso wa dunia mwamba joto wa kuyeyuka huitwa "magma" badala ya lava.

Lava inatoka nje kwa kawaida penye volkeno wakati wa mlipuko. Ikipoa inakuwa mwamba imara.

Wakati wa kutoka hali yake ni kiowevu yenye halijoto kati ya 600°C hadi 1200 °C. Katika hali hii inasambaa nje ya shimo la kasoko. Mwendo wake hutegemea na mnato wake yaani kama hali yake ni zaidi majimaji au ujiuji. Kadiri inavyoenea mbali na kasoko inapoa na kuwa mwamba.