Khalid Abdel Nasser

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Khalid Abdel Nasser ( Arabic , pia imeandikwa Khalid 'Abd al-Nasir; 13 Desemba 194915 Septemba 2011) [1] Ni mtoto wa kiume mkubwa wa Rais wa pili wa Misri Gamal Abdel Nasser na mkewe Tahia Kazem .

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Khalid (wa pili kutoka kushoto) na baba yake Gamal Abdel Nasser, dada Mona (kushoto) na Abdel Hamid (kulia), 1956

Nasser alizaliwa mwaka 1949. [2] Ali mhitimu Chuo Kikuu cha Cairo na Chuo Kikuu cha Cambridge ambapo alisomea uhandisi wa ujenzi. [2]

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Katikati ya miaka ya 1990 kufuatia vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iraq, Nasser alipokea vocha za mafuta za Saddam Hussein zenye thamani ya dola milioni 16.6 za mpango wa Mafuta kwa Chakula, zaidi ya mtu mwingine yeyote nchini Misri, kulingana na orodha ya wanufaika. Baadaye akawa profesa katika Kitivo cha Uhandisi cha Chuo Kikuu cha Cairo, kazi ambayo alishikilia kwa maisha yake yote.

Marejeleo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Khaled Abdel Nasser dies", Ahram Online, 15 September 2011. Retrieved on 15 September 2011. 
  2. 2.0 2.1 Sami Moubayed. "Nasser’s revolutionary spirit passed onto his children", Gulf News, 14 January 2018. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Khalid Abdel Nasser kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.