Kaspar Capparoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kaspar Capparoni

Kaspar Capparoni mjini Koloseo akiwa na Rex
Amezaliwa 1 Agosti 1964
Kazi yake mwigizaji wa filamu kutoka nchini Italia

Kaspar Capparoni (amezaliwa tar. 1 Agosti 1964) ni mwigizaji wa filamu kutoka nchini Italia.

Maisha ya mwanzo na filamu[hariri | hariri chanzo]

Capparoni alizaliwa mjini Roma, Italia. Kaspar Capparoni ameanza kujishughulisha na msuala ya ugizaji tangu akiwa na umri wa miaka 18. Alipata kushiriki katika moja kati ya filamu zilizoongozwa na Bw. Giuseppe Patroni Griffi. Kunako mwaka wa 1984, pia alipata kuonekana katika filamu ya Phenomena, iliyoongozwa na mtaalamu Dario Argento. Kaspar, pia amepata kucheza katika mafilamu kibao yaliyomaarufu katika ulimwengu huo. Filamu hizo ni pamoja na:

Pia amepata kufanya kazi katika vipindi kadhaa vya televisheni, ambavyo vinajumlisha: tamthiliya ya Ricominciamo (2000, mfululizo mdogo wa katika TV), Piccolo mondo antico (mfululizo mdogo wa katika TV), Incantesimo 4 (2001), Elisa di Rivombrosa (2003), La caccia (2005, mfululizo mdogo wa katika TV uliongozwa na Massimo Spano, akiwa kama adui wa Alessio Boni), na Capri (2006,mfululizo mdogo wa katika TV).

Kunako 2007, amecheza kama mhusika mkuu katika mfululizo mdogo wa Donna Detective ambayo imeongozwa na Cinzia TH Torrini. Mnamo mwaka wa 2008, pia alishiriki katika filamu ya Inspector Rex, ikiwa chini ya uongozi wake Marco Serafini, pia katika mfululizo wa Capri 2 iliyoongozwa na Andrea Barzini na Giorgio Molteni.

Kaspar Capparoni akiwa pamoja na Denise Zich na Martin Weinek.

Filamu[hariri | hariri chanzo]

Televisheni[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kaspar Capparoni kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.