Julian Huxley

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Julian Huxley

Sir Julian Sorell Huxley (22 Juni 188714 Februari 1975) alikuwa mwanabiolojia na mwandishi kutoka nchi ya Uingereza. Anajulikana hasa kwa maandishi yake ya kisayansi aliyojaribu kuyafanya yaeleweke na watu wengi wa kawaida. Pia alikuwa mkurugenzi wa kwanza wa UNESCO. Alipewa cheo cha Sir cha Uingereza mwaka wa 1958.

Huxley alizaliwa ndani ya familia maarufu. Kwa mfano, kaka yake ni mwandishi Aldous Huxley, na kaka mwingine ni mwanabiolojia Andrew Huxley, mshindi wa Tuzo ya Nobel; baba yake ni mwandishi na mhariri Leonard Huxley. Tena, babu yake aliyemzaa mamake ni mwanabiolojia T. H. Huxley, aliyefanya kazi na kumsaidia Charles Darwin.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:

Insha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Clark, Ronald, W. 1968. "The Huxleys". McGraw-Hill
  • Huxley, J., 1957. "Transhumanism". Angalia kiungo cha insha hiyo huko juu.
  • Huxley, J., 1970. Memories. George Allen & Unwin, London.
  • Kevles, D. J., 1985. In The Name Of Eugenics. University of California Press.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Julian Huxley kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.