Joseph Kony
Joseph Kony (alizaliwa mwaka 1961 hivi) ni kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Lord's Resistance Army (LRA), ambalo limejihusisha na kampeni za ghasia likiwa na azma ya kuanzisha serikali inyoongozwa na viongozi wa dini nchini Uganda, kundi hili liandai limejengeka kwenye misingi ya Biblia ya Kikristo na amri kumi. Kundi la LRA ambalo lilijulikana kwa vitendo vyake dhidi ya wenyeji wa Uganda Kaskazini, limeteka nyara takribani watoto 30,000 na kusababisha watu milioni 1.6 kukimbia makazi yao tangu uasi wao ulipoanza mwaka 1986. [1] [2] [3]
Wasifu
Joseph Kony alizaliwa mwaka 1961 katika kijiji cha Odek, kinachopatikana mashariki mwa Gulu kaskazini mwa Uganda, wazazi wake walikuwa wakulima. Aliwapenda wadogo zake lakini walipomkosea aliwaadhibu. [4] Katika ujana wake, Joseph Kony alifunzwa kuwa mganga wa kijiji na kaka yake, Benon Okello, na huyo alipoaga alichukua kikamilifu wajibu wa kuwa mganga wa kijiji. [5] Alipokosewa alipendela kupigana badala ya maelewano kwa njia ya mazungumzo. Akiwa shuleni alitaniwa kwa ukubwa wake na walimu walimpa wakati mgumu kwa sababu hakuonekana muerevu sana. Baba yake alikuwa mteandakazi wa mungu katika Kanisa Katoliki na mama yake alikuwa Mwanglikana, Kony alikuwa alatare kwa miaka kadhaa. Aliacha kwenda kanisani akiwa na umri wa karibu miaka 15. [4] Aliacha masomo yake shule ya upili na alipata umaarufu mwezi wa Januari mwaka 1986, akiwa na miaka ishirini na kitu hivi. Kundi lake lilikuwa moja ya makundi makubwa yaliyoibuka huko Acholi wakati wa vuguvugu maarufu la Roho Mtakatifu lililoongozwa na Alice Auma (aka Lakwena). Hata hivyo kulikuwa na mgogoro miongoni mwa Wacholi walionung'unikia kupoteza uashawishi wao baada ya Rais Tito Okello aliyekuwa Muacholikupinduliwa na Yoweri Museveni na jeshi lake la National Resistance Army (NRA) wakati wa Vita vya msituni vya Uganda vilivyoisha mwaka 1986.
Mwanzoni, kundi la Kony's liliitwa United Holy Salvation Army (UHSA) na halikuchukiliwa kama tisho na NRA. Kufikia mwaka 1988, baada ya mkataba kati ya NRA na Uganda People's Democratic Army kuongeza makundi yake mengine ya wapiganaji pamoja na kusajili watoto kwa nguvu kulilifanya kundi la United Holy Salvation Army kuwa jeshi lililoogofya. Askarijeshi wake wengi walikuwa watoto. Inakadiriwa kuwa amechukuwa watoto zaidi ya 104.000 wavulana na wasichana tangu LRA ilipoanza kupigana mwaka 1986. MMara nyingi aliua jamaa na majirani wa watoto hawa alipokuwa akiwateka na kuwalazimisha wapigane katika jeshi lake. Kamanda wa kundi lilosalia la UPDA alikuwa Odong Latek, ambaye alifanikiwa katika kumshawishi Kony atumie mbinu za kisasa za kijeshi kinyume na majaribio ya awali ambayo yalihusu mashambulizi ya mslaba na kutumia maji matakatifu. Mbinu hii mpya ilifanikiwa na UHSA mapigano madgomadogo lakini waliweza kuwashinda NRA. Baada ya ushindi huu NRA ililipiza kizazi kwa kudhoofisha kundi la Kony kisiasa na kampeni iliyoitwa Oparation North.
Kufikia mwaka 1992 alilipa hilo kundi jiypa la Muungano wa Jeshi la Kikristo la Demokrasia na ni katika wakati huu ndiyo waliowateka nyara wasichana 44 kutoka shule za upili za Sacred Heart Secondary na St. Mary's Girls School Operation North iliharibu kabisa kile kingekuwa wanamugambo wa Lord's Resistance Army,hata hivyo, ingawa idadi yao ilipungua kutoka maelfu hadi mamia waliendelea kuwavamia raia na washirika wa NRA.
Mazungumzo ya Bigombe ya mwaka 1993 yalifunua mengi kumhusu Joseph Kony. Betty Bigombe alikumbuka kwamba mara ya kwanza alikutana na Kony na wafuasi wake walitumia mafuta kujikinga na risasi na pepo mbaya. [6] Katika barua ilyohusu mazungumzo ya baadaye Kony pia alieleza kwamba sharti angetafuuta ushauri kutoka kwa Roho Mtakatifu. Mazungumzo yalipoanza walisisitiza kwamba viongozi wa dini washirikishwe na walifungua mkutano kwa maombi yaliongozwa na Mkurugenzi wa Masuala ya Dini wa LRA Bw. Jenaro Bongoni. Hatimaye katika mazungumzo ya amani ya mwaka 1994 Kony aliingia huku wanaume waliovaa majoho wakiwa mbele yake wakimyumyizia maji takatifu. [7]
Juhudi nyingi za kimataifa za kuleta amani na kukomesha utekaji nyara wa watoto na Kony na Wanamugambo wa kundi lake la Lord's Resistance Army zilifanyika kati ya 1996 na 2001. Juhudi zote zilishindwa kumaliza utekaji nyara wa watoto, ubakaji, askari-jeshi watoto mauji ya raia ikiwemo usambuliaji wa kambi za wakimbizi. Baada ya shambulizi la tarehe 11 Septemba Marekani ilitangaza rasmi wanamgambo wa Lord's Resistance Army kuwa kundi la kigaidi na Joseph Kony kuwa gaidi. [8]
Josph Kony alifikiriwa kuwa mtu mwenye pepo; amesawiriwa kama ama kma Masihi au shetani. Alizuru mara kadhaa milima ya Ato nchini Uganmda. Inadaiwa kuwa angekwea hadi kileleni cha milima na kulala huko kwenye jua kali kwa siku kadhaa. Angefunikwa na kundi la kumbikumbi wekundu ambao waliing'ata ngozi yake kwa undani. Mafuta kutoka mti uitwao Yao ilipakwa mwilini mwake. Kisha aliingia kwenye pango na kushinda huko pekee kwa majuma kadhaa. Alichowaamuru watoto wafanye kilikuwa kitu cha upuzi- aliwaambia kuwa iwapo wangechora mslaba kwenye vifua vyao na mafuta wangekingwa kutoka kutoka kwa risasi. [4] Kony anasisitiza kwamba wanamugambo wa Lord's Resistance Army wanapigania Amri Kumi. "Ndiyo, tunapigania Amri Kumi," Je, ni vibbaya? siyo kukiuka haki za binadamu. Na amri haikutolewa na Joseph. Haikutolewa na LRA. la, amri hiyo ilitolewa na Mungu. " [9]
Mashtaka rasmi
Lord's Resistance Army insurgency |
---|
Events
|
Related articles
Lord's Resistance Army |
Tarehe 6 Oktoba 2005 Mahaka ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilitoa vibali vya kukamtwa kwa wanamugambo watano wa kundi la Lord's Resistance Amy kwa uhalifu dhidi ya haki za binadamu kufuatia kufunguliwa mashitaka. Siku iliyofuata waziri wa ulinzi wa Uganda Amama Mbabazi alidokeza kuwa Joseph Kony, naibu wake Vincent Otti na makamanda wa Raska Lukwiya, Okot Odiambo na Dominic Ongwen walikuwa miongoni mwa wale ambao vibali vyao vya kukamtwa vilitolewa. Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi, jeshi la Uganda lilimua Lukwiya tarehe 12 Agosti 2006. [10]
Juma moja baadaye, tarehe 13 Oktoba, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ICC Luis Moreno Ocampo alitoa maelezo kuhusu mashitaka yaliyomkabili Kony. Kuna jumla ya mashtaka 33, 12 yakiwa ni uhalifu dhidi ya haki za binadamu, ambayo ni pamoja na mauaji, utumwa, utumwa wa ngono na ubakaji. Kuna mashitaka mengine 21 ya uhalifu wa kivita ambayo ni pamoja na mauaji, ukatili kwa raia, ushambulizi wa kimakusudi kwa raia, uporaji mali, ubakaji na kusajili watoto kwa nguvu katika vikosi vya waasi. Ocampo alisema kwamba "Kony aliwateka wasichana kuwatoa kama zawadi kwa makamanda wake."
Jeshi la Uganda limejaribu kumua Kony kwa shutuma za Upinzani .
Tarehe 31 Julai 2006, Kony alikutana na viongozi kadhaa kitamaduni, kisiasa, na viongozi wa dini kutoka Kaskazini mwa Uganda mafichoni mwake katika msitu wa kondo kuzungumzia vita. Siku iliyofuata, 1 Agosti, alivuka mpaka na kuingia Sudan kuzungumza na Makamu wa Rais wa Kusini mwa Sudan Riek Machar. Baadaye Kony aliwaambia waandishi wa habari kwamba hakuwa tayari kufika mbele ya mahakama ya ICC kujibu mashitaka kwa kuwa hajafanya lolote baya.
Tarehe 12 Novemba 2006 Kony alikutana na Jan Egeland, Umoja naibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura. Kony aliambia shirika la habari la Reuters: "Hatuna watoto wowote. tunawapiganaji tu. [11]
Tarehe 28 Agosti mwaka 2008, wizara ya fedha ya Marekani ilimuorodhesha Kony miongoni mwa kundi la "magaidi wa kipekee duniani" kundi ambalo huwa na adhabu za kifedha na adhabu. Haijulikani iwapo Kony ana miliki au hamilki rasilimali yoyote amabyo inaathiriwa na maelezo yaliyotolewa.
25 Desemba 2008, kwa mujibu wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa, waasi wa Lord's Resistance Army (LRA) waliwaua watu 189 na kuteka nyara watoto 120 wakati wa sherehe iliyofadhiliwa na Kanisa Katoliki huko Faradje, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Desemba 2008, jeshi la Kongo, pamoja na vikosi vya jeshi la Uganda na Sudan, vilivamia waasi wa LRA wakiwa na lengo la kuwanyang'anya silaha waasi wa LRA.
Tanbihi
- ↑ Flight of the child Soldiers
- ↑ BBC News - Mjube wa Umoja wa mataifa akutana na kiongozi wa waasi
- ↑ Buteera, Richard. The Reach Of Terrorists Financing And Combating It-The Links Between Terrorism And ordinary Crime. International Society of Prosecutors. Washington, DC. 12 Agosti 2003. [1] Ilihifadhiwa 27 Aprili 2007 kwenye Wayback Machine.
- ↑ 4.0 4.1 4.2 Jimmie Briggs "Innocents Lost: When Child Soldiers Go to war" 2005 s. 105-144
- ↑ Petro Eichstaedt, First Kill Your Family: Child Soldiers of Uganda and the Lord's Resistance Army, s. 206
- ↑ The Woman Behind Uganda's Peace Hopes- Betty Bigombe Put life on Hold to Interced in Northern War [2]
- ↑ BBC - Profile: Ugandan rebel Joseph Kony
- ↑ Philip T. Reeker (6 Desemba 2001). [https://web.archive.org/web/20020202195601/http://www.state.gov/r/pa/prs/ps/2001/6695.htm "Statement on the Designation of 39 Organizations on the USA PATRIOT Act's �Terrorist Exclusion List�"]. U.S. Department of State. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2002-02-02. Iliwekwa mnamo 2009-12-12.
{{cite web}}
: replacement character in|title=
at position 75 (help) - ↑ "I wil use the Ten Commandments to liberate Uganda". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-11-17. Iliwekwa mnamo 2009-12-12.
- ↑ "Ugandan army kills senior rebel'." BBC News. 13 Agosti 2006. 15 Februari 2007. [3]
- ↑ Kony told Reuters: "Hatuna watoto wowote tunawapiganaji pekee. [4]
Marejeo
- Green, Matthew (2008). The Wizard of the Nile: The Hunt for Africa's Most Wanted. Portobello Books. ISBN 978-1846270307.
{{cite book}}
: Cite has empty unknown parameter:|coauthors=
(help) - Briggs, Jimmie (2005). The Innocents Lost: When Child soldiers Go to war. Basic Books.
{{cite book}}
: Cite has empty unknown parameter:|coauthors=
(help)
Viungo vya nje
- Girl Soldiers-The cost of survivla in Northern Uganda Ilihifadhiwa 23 Mei 2012 kwenye Wayback Machine. Mtandao wa Habari za Wanawake - WNN
- "I want peace talks to resume" Ilihifadhiwa 1 Januari 2011 kwenye Wayback Machine. Mahojianao na Kony kwenye Radio France Internatinale English Service 22 Juni 2008
- Nataka amani lakini Museveni ndiye shida, asema Kony, Ilihifadhiwa 31 Machi 2003 kwenye Wayback Machine. makala ya mzungumzo ya Kony kwa njia ya simukwenye shoo ya redio ya mazungumzo ya siasa kwenye radi ya Mega Radio itangazayo kutoka Gulu tarehe 28 Desemba 2002.
- Mtoto wa kwanza wa Kony auawa Ilihifadhiwa 3 Mei 2008 kwenye Wayback Machine. New Vision,8 Julai 2005
- Hague Justice Portal: Joseph Kony Ilihifadhiwa 19 Desemba 2011 kwenye Wayback Machine.
- J. Carter Johnson, Deliver Us from Kony, Christanity Today, Januari 2006
- Sam Farmar, Uganda rebel leader breaks silence (mahojiano yaliyotolewa kwenye tuvuti katika kwa muundo wa MP3), BBC Newsnight, tarehe 28 Juni 2006, pia Google Video Ilihifadhiwa 29 Juni 2011 kwenye Wayback Machine.
- Ruud Elmendorp's video interview with Joseph Kony Ilihifadhiwa 17 Oktoba 2006 kwenye Wayback Machine. katika Rocketboom 16 Agosti 2006
- Ochola John, Mhasiriwa wa LRA: 'siwezi kusahau na kusamehe', BBC, tarehe 29 Juni 2006
- Julia Spiegel project discusses efforts to kill Joseph Kony Bloggingheads TV diavlog Jumapili 11 Januari 2009