Joseph Hill
Joseph Hill (22 Januari 1949 – 19 Agosti 2006) alikuwa mtunzi na mwimbaji wa Reggae toka nchini Jamaika. Alianza muziki katika kundi lijulikanalo kama The Soul Defender lililokuwa na makazi yake kitongoji cha St Catherine. Baadaye akaanzisha kundi la Culture akiwa na Telford Nelson na Albert Walker. Mwaka 1977 walitoa wimbo uliovuma sana uitwao Two Sevens Clash ambao ulizungumzia herufi mbili za 7 katika mwaka 1977. Hadi sasa Joseph Hill na wenzake wametoa album 22. Falsafa ya nyimbo za Joseph Hill ni ya kimapinduzi na kiroho inayopinga utumwa na ukosefu wa maadili na ucha mungu. Joseph Hill ni muumini wa imani na utamaduni wa Kirastafari. Katika wimbo wake wa wa PAY DAY anauliza ni lini watu walioumizwa na utumwa watalipwa. Pia amepinga aina zote za ukoloni na kumzumgumzia Chistopher Columbas kama muongo kwa kusema kwamba amegundua visiwa vya Jamaika ambavyo vilikuwapo tayari na watu. Joseph Hill pia anaenzi kitabu Bibilia anachoamini kuwa ni kitakatifu na amekuwa akitumia mistari na manabii toka kwenye Biblia kwenye nyimbo zake, kwa mfano wimbo wake kuhusu nabii Eliya.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti ya kundi la Culture Ilihifadhiwa 20 Machi 2007 kwenye Wayback Machine.