Joanna Fiodorow

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Joanna Fiodorow akiwa Poznań mwaka 2021..

Joanna Fiodorow (amezaliwa 4 Machi 1989) ni mwanariadha wa Polandi aliyebobea katika utupaji nyundo.

Mnamo mwaka 2010 alishinda medali ya shaba kwenye mashindano ya Uropa kwa kurusha kwa umbali wa mita73.67 .[1]

Alishindana katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 2012 huko London na michezo ya Olimpiki ya mwaka 2016 huko Rio , na ailshika nafasi ya 9 katika fainali zote mbili.[2]

Kutupa kwake bora zaidi ni umbali wa mita 75.09, aliyoipata mnamo mwaka 2017 huko Cetniewo.

Mwaka 2012 alifundishwa na kocha aitwaye Czeslaw Cybulski. [3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Wlodarczyk throws beyond 80 metres in Cetniewo | REPORT | World Athletics". www.worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-10-02. 
  2. "Joanna Fiodorow Bio, Stats, and Results | Olympics at Sports-Reference.com". web.archive.org. 2020-04-18. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-04-18. Iliwekwa mnamo 2021-10-02. 
  3. "Fiodorow and Michalski the standouts in Bydgoszcz | NEWS | World Athletics". www.worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-10-02.