Isaka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Abrahamu anazuiliwa na Mungu asimtoe Isaka kama sadaka
Uchongaji wa Andrea Mantegna kwenye altare mjini Mantua (mnamo 1461)

Isaka (kwa Kiebrania יצחק) ni jina la mwana wa Abrahamu anayetajwa katika Biblia ya Kiebrania, ambayo ni sehemu ya Biblia ya Kikristo (Agano la Kale).

Habari zake zinapatikana hasa katika kitabu cha Mwanzo 21:1-22;1 n.k. na 24;1-28 n.k.

Kufuatana na habari za kitabu hicho Abrahamu alimzaa na mke wake Sara akiwa mwana wake wa pili baada ya Ismaeli aliyemwahi kuzaa na mjakazi Hagar.

Katika Biblia anatazamiwa kama mrithi halali wa Abrahamu pamoja na kupokea baraka kutokana na agano la Mungu na ukoo wa babake.

Isaka alipokuwa mtoto bado aliokolewa na malaika kwenye altare alipoelekea kuchinjwa na baba yake kama sadaka .

Alimwoa Rebeka na kuzaa naye mapacha Esau na Yakobo.

Alipoaga dunia alizikwa kwenye pango la Makhpela karibu na mji wa Hebron.

Isaka anatajwa pia katika Kurani ya Uislamu.

[hariri] Viungo vya Nje

Saint-stub-icon.jpg Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Isaka kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.