Nenda kwa yaliyomo

Hifadhi ya Ngorongoro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Makundi ya wanyamapori katika kasoko.
Ramani ya eneo.
Eneo la Ngorongoro lipo kaskazini mwa Tanzania.
Ndani ya kasoko.

Hifadhi ya Ngorongoro (kwa Kiingereza: "Ngorongoro Conservation Area") ni hifadhi ya taifa kaskazini mwa Tanzania inayojulikana kote duniani, hasa baada ya kuorodheshwa na UNESCO kati ya mahali pa Urithi wa Dunia.

Kiini chake ni eneo la kasoko kubwa lenye umbali wa takriban kilomita 180 kutoka Arusha.

Kuna jumla ya wanyamapori wakubwa takriban 25,000, wakiwa pamoja na vifaru, viboko, nyumbu, pundamilia, nyati, simba, fisi na chui.

Bidii kubwa zaidi ya kulinda wanyama aina ya vifaru zinahitajika haraka kwa sababu idadi ya wanyama hao inazidi kupungua.

Mabaki ya zamadamu katika Olduvai Gorge yanaonyesha kwamba wanyama hao waliokoma walikuweko tangu miaka milioni 3 iliyopita.

Mwaka 1979 Ngorongoro ilipokewa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO upande wa uasilia.

Katika sekta ya utalii, ambayo nchi kama nchi huitegemea kwa kiasi fulani, ni muhimu serikali iandae miundombinu, hasa barabara zenye ubora wa hali ya juu, ili zitumike kwa muda mrefu na kuboresha sekta nyingine.

Kwa sababu ya aina mbalimbali za wanyama walioko, kasoko ya Ngorongoro inafahamika kama kivutio cha utalii duniani.
Mandhari ya kasoko ya Ngorongoro.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  • Ngorongoro Conservation Area Ilihifadhiwa 15 Novemba 2008 kwenye Wayback Machine. at the UNEP World Conservation Monitoring Centre
  • Deocampo, D.M., 2004. Hydrogeochemistry in the Ngorongoro Crater, Tanzania, and implications for land use in a World Heritage Site. Applied Geochemistry, volume 19, p. 755-767
  • Deocampo, D.M., 2005. Evaporative evolution of surface waters and the role of aqueous CO2 in magnesium silicate precipitation: Lake Eyasi and Ngorongoro Crater, northern Tanzania. South African Journal of Geology, volume 108, p. 493-504.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  • Ngorongoro Conservation Area Authority Ilihifadhiwa 23 Juni 2015 kwenye Wayback Machine.
  • Tanzania Tourist Bureau Ilihifadhiwa 13 Januari 2010 kwenye Wayback Machine.
  • "UNEP-WCMC World Heritage Site Datasheet" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (pdf) mnamo 2012-09-01. Iliwekwa mnamo 2015-07-09.
  • UNESCO World Heritage Site Datasheet