Hagia Sophia
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hagia Sophia ni jina la kanisa kubwa mjini Istanbul - Konstantinopoli lililobadilishwa kuwa msikiti tangu 1453 na kuwa makumbusho mwaka 1934. Jina latokana katika Kigiriki Ἅγια Σοφία ("hekima takatifu") na kwa Kituruki inaitwa Ayasofya.
Ujenzi wa kanisa ulianzishwa mwaka 532 na Kaisari Justinian I mtawala wa Roma ya Mashariki au Ufalme wa Byzanti. Alitaka kuwa na kanisa kubwa duniani akafaulu kwa sababu Hagia Sofia ilikuwa ukumbi mkubwa duniani hadi mwaka 1520. Jengo lilikamilishwa baada ya miaka mitano na Justinian alipoingia mara ya kwanza aliita "Suleimani nimekushinda" akimfikiria mfalme Suleimani wa Israeli ya Kale aliyejenga hekalu ya Yerusalemu.
Mwaka 1453 Waturuki Waislamu waliteka mji wa Konstantinopoli na kuifanya mji mkuu wa Dola la Osmani. Hagia Sofia likabadilishwa kuwa msikiti na Waturuki wakatamka jina la kigiriki kama "Ayasofya". Jengo la kanisa likaongezekwa minara minne ya mtindo wa Kiislamu.
Baada ya anguko la Waosmani katika vita kuu ya kwanza ya dunia kiongozi wa taifa Kemal Atatürk akaamuru jengo liwe makumbusho.
[hariri] Viungo vya Nje
- Hagia Sophia Audioguide visit map, Audioguide Seslirehber Hagia Sophia
| Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hagia Sophia kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |