Gali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Gali (Gallium)
Fuwele za Gali tupu
Fuwele za Gali tupu
Jina la Elementi Gali (Gallium)
Alama Ga
Namba atomia 31
Mfululizo safu Metali
Uzani atomia 69.723
Valensi 2, 8, 18, 3
Densiti 5.91 g/cm³
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 302.9146  K (29.7646 °C)
Kiwango cha kuchemka 2477 K (2204°C)
Asilimia za ganda la dunia 1 · 10-3 %
Hali maada mango

Gali ni elementi. Namba atomia yake ni 31 kwenye mfumo radidia na uzani atomia ni 69.723.

Ni metali haba na laini yenye rangi ya kifedha-buluu. Kwa halijoto ya duni ni mango kechu lakini huyeyuka tayari ikifikia kiwango cha 29 °C hivyo itayeyuka mkononi.

Hupatikana katika mitapo za boksiti na zinki.

Kampaundi zake hutumiwa kama nusupitisho katika teknolojia ya diodi.

Jina limetolewa na mwanakemia Mfaransa Paul Emile Lecoq de Boisbaudran aliyefumbua elementi hii mara ya kwanza mwaka 1875. "Gallium" larejea jina la "Gallia" ambalo ni jina la Kilatini la Ufaransa. Wengine huona ya kwamba alitaka kuweka kumbukumbu ya jina lake yeye mwenyewe kwa sababu "Lecoq" lamaanisha "jogoo" ambayo kwa Kilatini ni "gallus".

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.