Fisi-maji ni wanyama wa maji baridi au wa bahari (spishi mbili) wa nusufamilia Lutrinae katika familia Mustelidae. Wanyawa hawa wana mwili mrefu na mwembamba wenye mkia mrefu na manyoyo laini. Fisi-maji hushinda takriban maisha yao yote majini au baharini. Huogelea kwa kutumia miguu yao yenye ngozi kati ya vidole. Mkia hutumika kwa kupiga mbio umbali mdogo. Spishi za maji baridi hula samaki hasa lakini pia vyura, kasa wa maji baridi, mabata wadogo, panya na wadudu iwapo hakuna samaki wengi. Fisi-bahari wanastahabu invertebrata wa bahari kama kaa, kamba, uduvi, samakigamba, konokono wa bahari na chani, lakini samaki pengine pia. Huzaa watoto 1-5. Spishi za maji baridi huchimba au hutafuta tundu au mti uliobopa mara nyingi lakini fisi-bahari huzaa majini.
Spishi za Afrika [hariri]
Spishi za mabara mengine [hariri]
- Aonyx cinerea, Fisi-maji Mashariki (Oriental Small-clawed Otter)
- Enhydra lutris, Fisi-bahari Kaskazi (Sea Otter)
- Lontra canadensis, Fisi-maji wa Amerika ya Kaskazini (Northern River Otter)
- Lontra felina, Fisi-bahari Kusi (Marine Otter)
- Lontra longicaudis, Fisi-maji wa Amerika ya Kusini (Neotropical River Otter)
- Lontra provocax, Fisi-maji wa Argentina (Southern River Otter)
- Lutra nippon, Fisi-maji wa Japani (Japanese Otter)
- Lutra sumatrana, Fisi-maji wa Sumatra (Hairy-nosed Otter)
- Lutrogale perspicillata, Fisi-maji Manyoya-laini (Smooth-coated Otter)
- Pteronura brasiliensis, Fisi-maji Mkubwa wa Amerika (Smooth-coated Otter)
Spishi za kabla ya historia [hariri]
- Algarolutra majori (Pleistocene ya Korsika na Sardinia)
- Sardolutra ichnusae (Mwisho wa Pleistocene ya Sardinia)
- Megalenhydris barbaricina (Mwisho wa Pleistocene ya Sardinia)
-
Fisi-maji mkubwa wa Afrika
-
-
-
-
Fisi-maji wa Amerika ya Kaskazini
-
-
Fisi-maji wa Amerika ya Kusini
-
-
Fisi-maji mkubwa wa Amerika