Fimbi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fimbi
Fimbi domo-jekundu kaskazi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Bucerotiformes (Ndege kama hondohondo)
Familia: Bucerotidae (Ndege walio na mnasaba na hondohondo)
Rafinesque, 1815
Ngazi za chini

Jenasi 4 na spishi ?? za fimbi:

Fimbi ni jina linalotumika kwa spishi ndogo za familia ya ndege Bucerotidae; spishi moja inaitwa kwembe au kwembekwembe pia. Spishi kubwa za familia hii zinaitwa hondohondo. Fimbi wana domo kubwa lakini lile halina aina ya pembe juu lake kama domo la hondohondo au pembe hii ni dogo sana. Domo linaweza kuwa jeusi, jekundu au njano. Isipokuwa fimbi wadogo, spishi za Afrika zinatokea savana kavu na spishi za Asia zinatokea misitu. Fimbi hula matunda, mbegu, wadudu, mijusi na panya.

Jike wa fimbi huyataga mayai 2-6 katika tundu ya mti au mwamba, pengine katika tundu ya kigong'ota au zuwakulu. Dume afunga mwingilio wa tundu kwa matope, mavi na nyama ya matunda. Awaletea jike na makinda chakula.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]