Fadhéla Dziria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fadhéla Dziria

Fadhéla Dziria jina kamili Fadhéla Madani Bent el-Mahdi (25 Juni, 1917 - 6 Oktoba, 1970) alikuwa mwimbaji wa nchini Algeria wa muziki wa Hawzi.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Fadhéla Dziria alizaliwa Algiers, [1] binti wa Mehdi Ben Abderrahmane na Fettouma Khelfaoui. Alisikika kwa mara ya kwanza akiimba kwenye redio nchini Algeria. Katika miaka ya 1930. Alianza kurekodi katika miaka ya 1940, nyimbo nyingi za kitamaduni. Alizunguka kuimba katika miji mingine, na alionekana kwenye filamu mbalimbali. Na baadae katika kazi yake, alionekana pia kwenye televisheni. [2]

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Fadhéla Madani aliolewa akiwa na umri wa miaka 13. Alifariki mnamo 1970, akiwa na umri wa miaka 53. Makaburi yake yapo kwenye Makaburi ya El Kettar . [2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "The Diva of Algiers Song, Fadhela Dziria" Mediterranean Memory (1991).
  2. 2.0 2.1 "Meriem Fekkai et Fadila Dziria" Chouf-Chouf (4 September 2014).