Elsie Kanza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Elsie Kanza

Amezaliwa
nchini Kenya
Nchi Tanzania
Kazi yake balozi mpya mteule wa Tanzania nchini Marekani kutoka mwaka 2021

Elsie Kanza (alizaliwa tar.) ni mwanauchumi Mtanzania aliyezaliwa Kenya. Elsie ni Mkurugenzi mkuu wa Jukwaa la Uchumi wa Nchi za Afrika (World Economic Forum[1]) tangu mwaka 2014.

Kwa mujibu wa mtandao wa Forbes alitajwa kama mmoja kati ya Wanawake 20 Vijana wenye Nguvu Afrika kwa mwaka 2011.[2]

Maisha yake[hariri | hariri chanzo]

Kanza alizaliwa nchini Kenya na wazazi wenye asili ya Tanzania, akapata elimu yake nchini Kenya na baadaye kuendelea na masomo nchini Marekani.

Kwa kipindi cha miaka 1997-2006, Elsie aliweza kupata shahada ya biashara na utawala wa kimataifa katika chuo kikuu cha United States International – Afrika, shahada ya uzamili ya sayansi ya fedha katika chuo cha Strathclyde na shahada ya uzamili katika sanaa ya maendeleo ya kiuchumi katika chuo cha Williams cha nchini Marekani.[3]

Ameweza kupata nafasi mbalimbali za uongozi ikiwa ni pamoja na kuwa mshauri wa masuala ya uchumi wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kwa miaka 2006-2011. Pia Ni balozi mteule wa Tanzania nchini Marekani. Ameteuliwa tarehe 17/08/2021 na kuapishwa tarehe 21/08/2021[4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.lionessesofafrica.com/blog/2016/5/18/quote-of-the-day-by-elsie-kanza
  2. https://www.forbes.com/sites/faraigundan/2013/06/17/meet-elsie-kanza-head-of-africa-at-the-world-economic-forum-on-delivering-on-africas-promise/#1268ca9e7fcc
  3. https://www.huffingtonpost.com/ebenezar-wikina/wef-africa-at-25-my-strol_b_8508140.html
  4. https://www.weforum.org/agenda/authors/elsiekanza/
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Elsie Kanza kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.