Ebele Ofunneamaka Okeke

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ebele Ofunneamaka Okeke
Amezaliwa 14 Juni 1948
jimbo la Anambra
Nchi Nigeria
Kazi yake Mhandisi wa Umma


Ebele Ofunneamaka Okeke, (alizaliwa Nnewi, jimbo la Anambra, 14 Juni 1948[1]) ni Mhandisi wa Umma nchini Nigeria na Mkuu wa zamani wa Huduma ya Uhandisi Nigeria. [2][3]

Elimu na kazi[hariri | hariri chanzo]

Alipata elimu yake ya sekondari katika shule ya wasichana ya Archdeacon Crowther Memorial iliyoko katika mji wa Elelenwo, huko Port Harcourt, ambapo alipewa vyeti vya Shule ya Afrika Magharibi (WASC) mwaka 1965. [4] Aliendelea na elimu ya Chuo Kikuu cha Southampton, huko England ambapo alipata Shahada ya Sayansi (B.Sc.) katika Uhandisi wa Umma mwaka 1971. [5] Ana Diploma ya Uzamili (PGD) katika maji ya chini kutoka katika Chuo Kikuu cha Loughborough. [6] Pia alipata Digrii ya Uzamili (PGD) katika Hydrology na Hydrogeology kutoka katika Chuo Kikuu cha London mwaka 1979. Kisha alirudi Nigeria kupata Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara (MBA) kutoka katika Chuo Kikuu cha Nigeria, katika mji wa Nsukka mwaka 2001.[7][8] Mnamo Machi mwaka 2007, alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Federal Ministry of Water Resources na baada ya miezi kadhaaa ya huduma akawa Mkuu wa Utumishi wa Umma wa Nigeria, na kumfanya kuwa mwanamke wa kwanza kuhudumu katika nafasi hiyo katika historia ya Nigeria.[9] Alishikilia wadhifa huu hadi mwaka 2008, wakati alipostaafu katika Utumishi wa Umma wa Nigeria.[10] Yeye ni mmoja wa Wahandisi wa Umma nchini Nigeria ambapo wamechangia sehemu kubwa katika maendeleo ya Uhandisi wa Umma nchini Nigeria.[11] Alianzisha chapisho la Abuja la Association of Professional Women Engineers of Nigeria (APWEN) Archived 23 Novemba 2020 at the Wayback Machine..[12] Alikuwa mmoja wa wajumbe sita waliowakilisha watumishi wa umma waliostaafu katika Mkutano wa Kitaifa mwaka 2014 nchini Nigeria.[13][14]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Women in Business: Ebele Okeke (CFR, OON)". Businessday NG (kwa en-US). 2019-11-08. Iliwekwa mnamo 2020-05-25. 
  2. "David Mark and the Nation, Articles - THISDAY LIVE". thisdaylive.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-12-07. Iliwekwa mnamo 2014-12-04.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help)
  3. Rufus Kayode Oteniya. "Male And Female He Created Them. And So, Whatz Gender Got To Do With It". nigeriavillagesquare.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-03-09. Iliwekwa mnamo 2022-03-16. 
  4. Thomson Reuters Foundation. "Thomson Reuters Foundation". trust.org. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-12-10. Iliwekwa mnamo 2022-03-16. 
  5. "I’ll bring more girls into engineering – Iniobong Usoro, APWEN president". Online Nigeria. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-06-17. Iliwekwa mnamo 2022-03-16. 
  6. "Financial Nigeria - Development and Finance". www.financialnigeria.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-01-02. 
  7. "Africa News Service articles from September 2007, page 220 | HighBeam Business: Arrive Prepared". business.highbeam.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-12-07. Iliwekwa mnamo 2018-01-02.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help) Archived 7 Desemba 2014 at the Wayback Machine.
  8. "The Unfolding Staff of Yar`Adua`s Presidential Office - Nigerian Muse". nigerianmuse.com. 
  9. Nigeria's Stumbling Democracy and Its Implications for Africa's Democratic ... 
  10. "Retired civil servants protest pension cuts". Vanguard News. 
  11. "Women in Business: Ebele Okeke (CFR, OON)". Businessday NG (kwa en-US). 2019-11-08. Iliwekwa mnamo 2020-05-25. 
  12. "Apwen Honours Best Female Science Students - Worldnews.com". wn.com. 
  13. "Confab: Delegate seeks ban on open urination - Premium Times Nigeria". Premium Times Nigeria. 
  14. Splendour and Marcus Articles. "Anyim names appointees to National Conference". Federal Government Of Nigeria. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-12-08. Iliwekwa mnamo 2014-12-04.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help)